Jumamosi asubuhi tarehe 08.06.2024
Isaya 37:8-14
8 Basi yule amiri akarudi, akamkuta mfalme wa Ashuru anafanya vita juu ya Libna; kwa maana alikuwa amesikia ya kwamba ameondoka, akaacha Lakishi.
9 Naye alisikia habari ya Tirhaka, mfalme wa Kushi, ya kwamba, Ametoka ili kupigana nawe; naye aliposikia hayo, akatuma wajumbe kwa Hezekia, kusema,
10 Mwambieni Hezekia, mfalme wa Yuda, maneno haya, mkisema, Asikudanganye Mungu wako unayemtumaini, akisema, Yerusalemu hautatiwa katika mikono ya mfalme wa Ashuru.
11 Tazama, umesikia habari ya mambo yote, ambayo wafalme wa Ashuru wamezitenda nchi zote, kwa kuziangamiza kabisa je! Utaokoka wewe?
12 Je! Miungu ya mataifa, ambao baba zangu waliwaangamiza, wamewaokoa? Gozani, na Harani, na Resefu, na wana wa Adini waliokuwa katika Telasari?
13 Yuko wapi mfalme wa Hamathi, na mfalme wa Arpadi, na mfalme wa mji wa Sefarvaimu, wa Hena, na wa Iva?
14 Basi Hezekia akaupokea waraka katika mikono ya wale wajumbe, akausoma; kisha Hezekia akapanda, akaingia katika nyumba ya Bwana, akaukunjua mbele za Bwana.
Chagueni mtakayemtumikia;
Baada ya kuivamia Yuda na kuitwaa, Hezekia analetewa ujumbe uliomjulisha kuwa isingewezekana Yuda kutwaliwa na Ashuru. Ukiendelea kusoma unaona Hezekia akiomba sala ndefu kwa Bwana, ombi lake likiwa ni rehema ya Bwana. Nabii Isaya baadaye anamtangazia msamaha toka kwa Bwana.
Kilichomleta Kristo ni kutuokoa. Kwa njia hiyo hutusamehe dhambi zetu bure. Ndiyo maana tunasema wokovu wetu ni kwa neema, maana ni bure. Neema ya Bwana ingalipo daima, na wokovu ni kwa wote. Chagua kumtumikia Bwana. Amina.
Jumamosi njema
Heri Buberwa