Alhamisi asubuhi tarehe 06.06.2024
1 Wafalme 18:17-21
17 Ikawa, Ahabu alipomwona Eliya, Ahabu akamwambia, Je! Ni wewe, Ewe mtaabishaji wa Israeli?
18 Naye akajibu, Si mimi niliyewataabisha Israeli; bali ni wewe, na nyumba ya baba yako, kwa kuwa mmeziacha amri za Bwana; nawe umewafuata mabaali.
19 Basi sasa upeleke watu, unikusanyie jamii ya Israeli katika mlima wa Karmeli, na wale manabii wa Baali mia nne na hamsini, na wale manabii wa Ashera mia nne, walao chakula mezani pa Yezebeli.
20 Basi, Ahabu akapeleka watu kwa wana wa Israeli wote, akawakusanya manabii pamoja katika mlima wa Karmeli.
21 Naye Eliya akawakaribia watu wote, akanena, Mtasita-sita katikati ya mawazo mawili hata lini? Bwana akiwa ndiye Mungu, mfuateni; bali ikiwa Baali ni Mungu, haya! Mfuateni yeye. Wale watu hawakumjibu neno.
Chagueni mtakayemtumikia;
Ahabu alikutana na Eliya, ni katika nchi iliyokuwa na njaa, na ukame. Ahabu anamuona Eliya kama mtaabishaji wa Israeli! Lakini Eliya anamwambia Ahabu kuwa njaa waliyo nayo ni kwa sababu waliziacha amri za Bwana na kuwafuata mabaali. Eliya katika kutaka kuuonesha ufalme wa Mungu, anamuelekeza Ahabu kuwakusanya jamii ya Israeli, manabii wa Baali, na wale wa Ashera.
Ujumbe wa Eliya kwa Ahabu ulikuwa ni kwamba njaa ilikuwa ni kwa sababu ya kuziacha amri za Bwana. Hapa tunapata ujumbe kuwa tunapomuacha Yesu tunakuwa hatuko salama, maana yeye ndiyo Mwokozi wetu na hatma yetu iko mikononi mwake. Tukichagua kumtumikia yeye (Yesu) tunakuwa salama. Amina.
Alhamisi njema
Heri Buberwa Nteboya
0784 968650