Date: 
05-06-2024
Reading: 
Yohana 7:40-52

Jumatano asubuhi tarehe 05.06.2024

Yohana 7:40-52

40 Basi wengine katika mkutano walipoyasikia maneno hayo, walisema, Hakika huyu ndiye nabii yule.

41 Wengine walisema, Huyu ndiye Kristo. Wengine wakasema, Je! Kristo atoka Galilaya?

42 Andiko halikusema ya kwamba Kristo atoka katika uzao wa Daudi, na kutoka Bethlehemu, mji ule alioukaa Daudi?

43 Basi kukaingia matengano katika mkutano kwa ajili yake.

44 Baadhi yao wakataka kumkamata, lakini hakuna mtu aliyenyosha mikono yake ili kumshika.

45 Basi wale watumishi wakawaendea wakuu wa makuhani na Mafarisayo. Nao wakawaambia, Mbona hamkumleta?

46 Wale watumishi wakajibu. Hajanena kamwe mtu ye yote kama huyu anavyonena.

47 Basi Mafarisayo wakawajibu, Je! Ninyi nanyi mmedanganyika?

48 Ni nani katika wakuu amwaminiye, au katika Mafarisayo?

49 Lakini makutano hawa wasioifahamu torati wamelaaniwa.

50 Akawaambia Nikodemo, (naye ni yule aliyemwendea zamani, maana ni mmoja wao),

51 Je! Torati yetu humhukumu mtu kabla ya kumsikia kwanza, na kujua atendavyo?

52 Wakajibu, wakamwambia, Je! Wewe nawe umetoka Galilaya!

Chagueni mtakayemtumikia;

Yesu alikuwa anafundisha kiasi kwamba ilifika hatua akawa anawashangaza watu, maana alionekana kuwa na upeo mkubwa. Inaonekana katika sura ya saba hiyo hiyo;

Yohana 7:14-15

14 Hata ikawa katikati ya sikukuu Yesu alikwea kuingia hekaluni, akafundisha.
15 Wayahudi wakastaajabu wakisema, Amepataje huyu kujua elimu, ambaye hakusoma?

Walisema kwamba ana pepo, yaani hawakumuamini. Wapo wachache waliomuamini. Tunasoma katika somo kuwa wapo wapo walipomuona Nabii, wengine wakisema ndiye Kristo. Lakini baadhi waliotumwa na Mafarisayo walitaka kumkamata, wakashindwa.

Kutomkamata Yesu kama walivyotumwa kunaweza kuwa na sababu tofauti. Labda walielewa mafundisho yake, au walishindwa. Lakini Injili inasema saa yake ilikuwa bado. 

Kikubwa ninachokiona ni walioshindwa kumkamata Yesu, baada ya kusikia neno lake. Kumbe Kristo anatujia kwa njia ya neno lake. Tuchague kumtumikia kwa kulishika neno lake. Amina

Jumatano njema 

 

Heri Buberwa