MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 24 MACHI, 2024
SIKU YA MITENDE
NENO LINALOTUONGOZA NI
SHANGILIENI BWANA ANAKUJA
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna Mgeni aliyetufikia kwa cheti.
3. Matoleo ya Tarehe 17/03/2024
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV.
5. Jumatano ijayo tarehe 27/03/2024 saa 11.00 jioni tutaendelea na ibada ya Kwaresma ambayo ndiyo itakuwa jumatano ya mwisho. Zamu za Wazee itakuwa ni kundi la Pili.
6. Uongozi wa Umoja wa wanawake unapenda kuwashukuru wanawake wote waliohudhuria ibada ya Maadhimisho ya pasaka jana tarehe 23/03/2024 Kijimbo Usharika wa Kitunda Kuu. Mungu awabariki sana.
7. Leo tarehe 24/03/2024 ni siku ya Mitende.
8. Uongozi wa Usharika pamoja na Kamati ya Afya wanamshukuru Mungu sana kwa kufanikisha Ibada ya Wazee kuanzia miaka 60 na kuendelea iliyofanyika jana tarehe 23/03/2024 hapa usharikani Azania Front Cathedral kuanzia saa 3.00 asubuhi iliyoambatana na Chakula cha Bwana.
9. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Upanga: Watatangaziana
- Mjini kati: Watatangaziana
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa ………………………………..
- Kinondoni: Kwa …………………….
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa …………………….
- Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Oysterbay, Masaki: Watashiriki ibada za jumatano hapa Kanisani
10. Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Pili.
11. RATIBA YA PASAKA
https://www.azaniafront.org/node/2338