Date: 
06-12-2023
Reading: 
Mathayo 21:1-11

Hii ni Advent 

Jumatano asubuhi tarehe 06.12.2023

Mathayo 21:1-11

1 Hata walipokaribia Yerusalemu, na kufika Bethfage, katika mlima wa Mizeituni, ndipo Yesu alipotuma wanafunzi wawili akiwaambia,

2 Enendeni mpaka kijiji kile kinachowakabili, na mara mtaona punda amefungwa, na mwana-punda pamoja naye; wafungueni mniletee.

3 Na kama mtu akiwaambia neno, semeni, Bwana anawahitaji; na mara huyo atawapeleka.

4 Haya yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na nabii, akisema,

5 Mwambieni binti Sayuni Tazama, mfalme wako anakuja kwako, Mpole, naye amepanda punda, Na mwana-punda, mtoto wa punda.

6 Wale wanafunzi wakaenda zao, wakafanya kama Yesu alivyowaamuru,

7 wakamleta yule punda na mwana-punda, wakaweka nguo zao juu yao, naye akaketi juu yake.

8 Watu wengi katika ule mkutano wakatandaza nguo zao njiani; na wengine wakakata matawi ya miti, wakayatandaza njiani.

9 Na makutano waliotangulia, na wale waliofuata, wakapaza sauti, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi; ndiye mbarikiwa, yeye ajaye kwa jina la Bwana; Hosana juu mbinguni.

10 Hata alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakisema, Ni nani huyu?

11 Makutano wakasema, Huyu ni yule nabii, Yesu, wa Nazareti ya Galilaya.

Bwana analijia Kanisa lake;

Jumapili iliyopita tulitafakari juu ya unabii wa Zekaria kuhusu ujio wa mfalme ambaye angewakomboa Israeli. Mstari huu ulituongoza;

Zekaria 9:9

Furahi sana, Ee binti Sayuni; Piga kelele, Ee binti Yerusalemu; Tazama, mfalme wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana wokovu; Ni mnyenyekevu, amepanda punda, Naam, mwana-punda, mtoto wa punda.

Kuingia Yerusalemu kwa shangwe Yerusalemu ulikuwa ni utimilifu wa unabii wa Zekaria kuhusu ujio wa Yesu Kristo. 

Kuingia Yerusalemu kwa shangwe ilikuwa ni hatua ya kukiendea kifo, hatua ambayo ilikamilika kwa Yesu kufufuka na kupaa mbinguni. Majira haya yatukumbushe kuwa Yesu alizaliwa kwa ajili yetu, akafa na kufufuka ili kutukomboa. Atarudi tena mara ya pili kwa utukufu, hivyo tujiandae kumpokea. Amina.

Jumatano njema 

 

Heri Buberwa 

Mlutheri