Date: 
06-09-2023
Reading: 
Luka 10:25-28

Jumatano asubuhi tarehe06.09.2023

Luka 10:25-28

25 Na tazama, mwana-sheria mmoja alisimama amjaribu; akisema, Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?

26 Akamwambia, Imeandikwa nini katika torati? Wasomaje?

27 Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako.

28 Akamwambia, Umejibu vema; fanya hivi nawe utaishi.

Jirani wetu;

Mwanasheria alimuuliza Yesu afanye nini ili aurithi uzima wa milele. Yesu katika kumjibu alimuuliza imeandikwaje katika Torati. Mwanasheria alijibu, na jibu lake ndiyo msingi wa somo la asubuhi ya leo;

Luka 10:27

Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako.

Aliyeuliza swali anarejea torati inayoelekeza kila mmoja kumpenda Mungu na jirani kama nafsi yake. Yesu alimwambia aliyejibu kuwa alijibu vema, akimtuma akafanye hivyo. Kwa njia hiyo, Yesu anatuagiza kumpenda Mungu na jirani zetu. Amina. 

Jumatano njema.

 

Heri Buberwa