Date: 
05-09-2023
Reading: 
Zekaria 8:16-18

Jumanne asubuhi tarehe 05.09.2023

Zekaria 8:16-18

16 Haya ndiyo mtakayoyatenda; kila mtu na aseme kweli na jirani yake; hukumuni kweli na hukumu ya amani malangoni mwenu;

17 wala mtu wa kwenu asiwaze mabaya moyoni mwake juu ya jirani yake; wala msipende kiapo cha uongo; maana hayo yote ndiyo niyachukiayo, asema Bwana.

18 Tena neno la Bwana wa majeshi likanijia, kusema,

Jirani wetu;

Nabii Zekaria analeta ujumbe wa Mungu kwa taifa lake, akiwausia watu kumcha Bwana na kuishi kwa mapenzi yake. Katika kuendeleza ujumbe huo, asuhuhi hii tunamsoma Zekaria akiwaambia watu kusema kweli kila mtu kwa jirani yake. Mtume Paulo alirejea ujumbe huu kwa waefeso;

Waefeso 4:25

Basi uvueni uongo, mkaseme kweli kila mtu na jirani yake; kwa maana tu viungo, kila mmoja kiungo cha wenzake.

Kumbe Nabii Zekaria anatukumbusha kuishi kwa upendo tukisema kweli, kila mtu kwa jirani yake, kama mtume Paulo alivyorejea ujumbe huu. Maisha yetu sisi kwa pamoja yanatakiwa kuakisi upendo, kila mmoja akiwa shahidi mwema kwa mwenzake. Wewe ni shahidi mwema kwa jirani yako?

Siku njema

 

Heri Buberwa