MATANGAZO YA USHARIKA TAREHE 27 AGOSTI, 2023
SIKU YA BWANA YA 12 BAADA YA UTATU
NENO LINALOTUONGOZA NI
MATUMIZI YA ULIMI
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti.
3. Matoleo ya Tarehe 20/08/2023
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV.
5. Leo tarehe 27/08/2023 tutashiriki Chakula cha Bwana. Washarika karibuni.
6. Umoja wa Wanawake Azania Front unawatangazia Wanawake wote semina itakayofanyika katika kituo chetu cha Kiroho Kiharaka tarehe 9 Septemba 2023 kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 10 jioni. Usafiri wa kuelekea Kiharaka utakuwepo hapa kanisani saa 12 kamili asubuhi. Ili kuweza kufanya maandalizi na usafiri tunaomba Wanawake wajiandikishe kupitia WhatsApp Group ya UWA au ofisini kwa Parish Worker.
7. NDOA. NDOA ZA WASHARIKA
KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 02/09/2023
SAA 8.00 MCHANA
- Bw. Mwemezi Rugabeza Mutembei na Bi. Dianarose Leons Lyimo
Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo.
8. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Oysterbay na Masaki: Kwa Bwana na Bibi Aron Ndasiwa
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mama Korosso
- Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Danford Mariki
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Mcharo
- Upanga: Kwa Bwana na Bibi George Kinyaha
- Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa Mama Elly Swai
9. Zamu: Zamu za wazeeni ni Kundi la Pili
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu,
Bwana ayabariki.