Date: 
05-08-2023
Reading: 
Ezra 9:10-15

Jumamosi asubuhi tarehe 05.08.2023

Ezra 9:10-15

10 Na sasa, Ee Mungu wetu, tuseme nini baada ya hayo? Maana tumeziacha amri zako,

11 ulizoziamuru kwa midomo ya watumishi wako, manabii, ukisema, Nchi ile, mnayoiendea ili kuimiliki, ni nchi ya uchafu, kwa sababu ya uchafu wa watu wa nchi zile, kwa ajili ya machukizo yao, yaliyoijaza tangu upande huu mpaka upande huu, kwa uchafu wao.

12 Basi, msiwape wana wao binti zenu, wala msitwae binti zao kuwa wake za wana wenu, wala msiwatakie amani wala kufanikiwa milele; ili mpate kuwa hodari, na kula wema wa nchi hiyo, na kuwaachia watoto wenu iwe urithi wa milele.

13 Na baada ya hayo yote yaliyotupata kwa sababu ya matendo yetu mabaya, na kwa sababu ya hatia yetu iliyo kuu, ikiwa wewe Mungu wetu hukutuadhibu kama tulivyostahili kwa maovu yetu, tena umetupa mabaki;

14 je! Tuzivunje tena amri zako, tukajiunge na watu wanaotenda machukizo hayo, kwa kuoana nao? Je! Usingekasirika nasi hata kutuangamiza kabisa, pasisalie mabaki yo yote, wala mtu wa kuokoka?

15 Ee Bwana, Mungu wa Israeli, wewe ndiwe mwenye haki, maana sisi tumesalia, mabaki yaliyookoka, kama hivi leo; tazama, sisi tupo hapa wenye hatia mbele zako; maana hapana mtu awezaye kusimama mbele zako kwa sababu ya jambo hili.

Wema wa Mungu watuvuta tupate kutubu;

Baada ya Israeli kuingia katika nchi ya ahadi, walifanya mambo ambayo yalikuwa chukizo kwa Bwana. Walikuta nchi imejaa uchafu, wakaendelea na uchafu huo (10). Walikutwa na mambo mabaya kwa sababu ya uovu wao. Walizivunja amri za Mungu kwa kuungana waovu.

Somo tulilosoma ni toba ambayo alifanya Ezra akimuomba Mungu awarehemu Israeli. Ukiendelea kusoma sura inayofuatia unaona Mungu akiwarehemu. Kumbe nasi tukitubu Mungu hutusamehe. Tubu dhambi zako usamehewe. Amina 

Heri Buberwa