Date: 
03-11-2021
Reading: 
Mathayo 11:11-15

Jumatano tarehe 03.11.2021, asubuhi.

Mathayo 11:11-15

11 Amin, nawaambieni, Hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji; walakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye.

12 Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.

13 Kwa maana manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana.

14 Na ikiwa mnataka kukubali, yeye ndiye Eliya atakayekuja.

15 Mwenye masikio, na asikie.

Mwenye haki ataishi kwa imani;

Yesu anafundisha akisema ufalme wa Mungu utatekwa na wenye nguvu. Nguvu hii siyo ya  kupigana au kubeba vitu vizito, au kwenda mwendo mrefu n.k ni kusimama katika kweli, hata ukibaki peke yako katika jambo  fulani, kama una uhakika jambo hilo ni kweli. Yesu anawataja Nabii Elia na Yohana Mbatizaji. Na mimi naongezea, Martin Luther. Tuwaangalie kwa ufupi;

1. Nabii Elia.

Alikemea watu katika Israeli kuabudu miungu ya Baali. Haikuwa rahisi, wengi waliona lakini walinyamaza. Elia aliamua kupaza sauti, hii ndiyo nguvu yenyewe.

2. Yohana Mbatizaji;

Alimkemea Herode akimwambia ndoa yake ilikuwa batili, maana alimchukua mke wa Filipo ndugu yake. Waliona wengi, lakini walinyamaza. Ilisababisha Yohana kukatwa kichwa, lakini ujumbe wake ulifika. Alipaza sauti. Hii ndiyo nguvu ya kuuteka ufalme wa Mungu.

3. Martin Luther

Alikataa mafundisho yasiyoendana na neno la Mungu kuhusu imani, haki, msamaha wa dhambi, hadi kwenda kinyume na viongozi wake kwa wakati huo, walioishia kumtenga. Uovu huu ulionekana kwa watawa wengi, lakini Luther alipaza sauti. Hii ndiyo nguvu ya kuuteka ufalme  wa Mungu, maana kwa sauti yake, sisi leo tunao msimamo kuhusu neno la Mungu kama aliokuwa nao yeye Martin Luther.

Nakuacha na swali;

Unayo nguvu ya kuuteka ufalme wa Mungu?

Siku njema.


WEDNESDAY 3RD NOVEMBER 2021, MORNING

MATTHEW 11:11-15 NIV

11 Truly I tell you, among those born of women there has not risen anyone greater than John the Baptist; yet whoever is least in the kingdom of heaven is greater than he. 12 From the days of John the Baptist until now, the kingdom of heaven has been subjected to violence,[a] and violent people have been raiding it. 13 For all the Prophets and the Law prophesied until John. 14 And if you are willing to accept it, he is the Elijah who was to come. 15 Whoever has ears, let them hear.

Read full chapter

Footnotes

  1. Matthew 11:12 Or been forcefully advancing

 

The just shall live by faith;

Jesus teaches that the kingdom of God will be captured by the powerful. This power is not about fighting or carrying heavy objects, or going long distances etc. It is standing in the truth, even if you are left alone in whatever situation, if you are sure that it is true. Jesus names the prophets Elijah and John the Baptist as examples. And I add, Martin Luther. Let's look at them briefly;

1. The prophet Elijah.

He rebuked the people of Israel for worshiping the gods of Baal. It was not easy, many noticed but remained silent. Elijah decided to speak out, this is the power itself.

2. John the Baptist;

He rebuked King Herod, saying that he had converted his brother’s wife unlawfully. Many had seen this, but remained silent. It caused John to be beheaded, but his message was sent. He spoke up. This is the power to seize the kingdom of God.

3. Martin Luther

He rejected the unscriptural teachings of faith, righteousness, forgiveness of sins, and even went against his leaders at that time, who ended up separating him. This evil was seen by many monks, but Luther cried out. This is the power to seize the kingdom of God, for by his voice, we today have the same position on the word of God as Martin Luther did.

I leave you with a question;

Do you have the power to capture the kingdom of God?

Good day.