Date: 
13-09-2022
Reading: 
Marko 3:31-35

Jumanne asubuhi tarehe 13.09.2022

Marko 3:31-35

[31]Wakaja mamaye na nduguze; wakasimama nje, wakatuma mtu kumwita.

[32]Na makutano walikuwa wameketi, wakimzunguka, wakamwambia, Tazama, mama yako na ndugu zako wako nje, wanakutafuta.

[33]Akawajibu, akisema, Mama yangu na ndugu zangu ni akina nani?

[34]Akawatazama wale walioketi wakimzunguka pande zote, akasema, Tazama, mama yangu na ndugu zangu!

[35]Kwa maana mtu ye yote atakayeyafanya mapenzi ya Mungu, huyo ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu.

Jirani yako ni nani?

Kila mwaka watu walikwenda Yerusalemu kwa sherehe za Pasaka. Familia ya Yesu walikwenda pia. Ikawa siku moja walipoenda, wakati wa kurudi wakagundua kuwa mtoto Yesu alikuwa amebaki Yerusalemu. Ndipo tunaona akikutwa hekaluni, ambapo ndugu zake walirudi kumchukua. Luka anaandika kwa urefu zaidi (Luka 2:41-52)

Yesu alipoambiwa kuwa ndugu zake walimtafuta, alisema waliokuwa wameketi kumzunguka ndiyo ndugu zake. Yesu hakuwakana ndugu zake. Injili ya Luka humtaja Yesu kuwatii wazazi wake;

Luka 2:51

[51]Akashuka pamoja nao mpaka Nazareti, naye alikuwa akiwatii; na mamaye aliyaweka hayo yote moyoni mwake.

Yesu alienda mbele zaidi akimaanisha wanaokaa na kujifunza kwake wakamfuata ndiyo ndugu zake. Yesu anatuita kufanya yaliyo mapenzi yake, ndipo tunakuwa ndugu zake, na ujirani wetu unakuwa mwema katika yeye.

Siku njema.