Date: 
17-02-2020
Reading: 
Mark 4:1-9  (Marko 4:1-9

MONDAY 17TH FEBRUARY 2020  MORNING                                                        

Mark 4:1-9 New International Version (NIV)

1Again Jesus began to teach by the lake. The crowd that gathered around him was so large that he got into a boat and sat in it out on the lake, while all the people were along the shore at the water’s edge. He taught them many things by parables, and in his teaching said: “Listen! A farmer went out to sow his seed. As he was scattering the seed, some fell along the path, and the birds came and ate it up. Some fell on rocky places, where it did not have much soil. It sprang up quickly, because the soil was shallow. But when the sun came up, the plants were scorched, and they withered because they had no root. Other seed fell among thorns, which grew up and choked the plants, so that they did not bear grain. Still other seed fell on good soil. It came up, grew and produced a crop, some multiplying thirty, some sixty, some a hundred times.”

Then Jesus said, “Whoever has ears to hear, let them hear.”

God’s grace is for everyone. We need God’s word to remind us of His abundant grace. Through hearing His word, God will grant us the ability to see it, believe it, rest in it, draw confidence from it, and share it.


JUMATATU TAREHE 17 FEBRUARI 2020  ASUBUHI                                     

MARKO 4:1-9

1 Akaanza kufundisha tena kando ya bahari. Wakamkusanyikia mkutano mkubwa mno, hata yeye akapanda chomboni, akakaa baharini, mkutano wote ulikuwako juu ya nchi kavu kando ya bahari.
Akawafundisha mambo mengi kwa mifano, akawaambia katika mafundisho yake,
Sikilizeni; Tazama, mpanzi alitoka kwenda kupanda;
ikawa alipokuwa akipanda, mbegu nyingine ilianguka kando ya njia, wakaja ndege wakaila.
Nyingine ikaanguka penye mwamba, pasipokuwa na udongo mwingi; mara ikaota kwa kuwa na udongo haba;
hata jua lilipozuka iliungua, na kwa kuwa haina mizizi ikanyauka.
Nyingine ikaanguka penye miiba; ile miiba ikamea ikaisonga, isizae matunda.
Nyingine zikaanguka penye udongo ulio mzuri, zikazaa matunda, zikimea na kukua, na kuzaa, moja thelathini, moja sitini, na moja mia.
Akasema, Aliye na masikio ya kusikilia, na asikie.

Neema ya Mungu imefunuliwa kwa watu wote. Tunahitaji neno la Mungu ili litukumbushe juu ya wingi wa neema yake. Kwa kulisikia na kulipokea neno lake, Mungu atatupa uwezo wa kuona, kuliamini, kupata pumziko ndani yake na kuwafundisha wengine.