Date: 
05-04-2017
Reading: 
Luke 23:8-12 (NIV)

WEDNESDAY 5TH APRIL 2017 MORNING                               

Luke 23:8-12 New International Version (NIV)

When Herod saw Jesus, he was greatly pleased, because for a long time he had been wanting to see him. From what he had heard about him, he hoped to see him perform a sign of some sort. He plied him with many questions, but Jesus gave him no answer. 10 The chief priests and the teachers of the law were standing there, vehemently accusing him. 11 Then Herod and his soldiers ridiculed and mocked him. Dressing him in an elegant robe, they sent him back to Pilate. 12 That day Herod and Pilate became friends—before this they had been enemies.

The Lord Jesus was arrested and falsely accused. He was questioned by the High priest and by King Herod and by the Roman official Pilate. He was mocked and abused and later crucified. Jesus went through all this suffering so that you and I can be saved and reconciled to God.

How do you treat Jesus? Do you appreciate what He did for you?  

JUMATANO TAREHE 5 APRILI 2017 ASUBUHI                      

LUKA 23:8-12

8 Na Herode alipomwona Yesu alifurahi sana, kwa sababu alikuwa akitaka sana kumwona tangu siku nyingi, maana amesikia habari zake, akataraji kuona ishara iliyofanywa na yeye. 
9 Akamwuliza maneno mengi, yeye asimjibu lo lote. 
10 Wakuu wa makuhani na waandishi wakasimama wakamshitaki kwa nguvu sana. 
11 Basi Herode akamfanya duni, pamoja na askari zake, akamdhihaki, na kumvika mavazi mazuri; kisha akamrudisha kwa Pilato. 
12 Basi siku ile ile Herode na Pilato walipatana kwa urafiki kwa maana hapo kwanza walikuwa na uadui wao kwa wao. 
 

Bwana Yesu Kristo alikamatwa na maadui. Alipelekwa  kuhukumiwa na kuulizwa maswali na Kuhani Mkuu, Mfalme Herode na Afisa wa Warumi, Pilato. Yesu alidharauliwa na kuhukumiwa kifo bila hatia. Yesu aliteswa sana na alikufa msalabani kwa ajili ya wewe na mimi. Yesu alikufa ili sisi tusamehewe na tupatanishwe na Mungu mtakatifu.

Je! Unamheshimu Yesu? Unamshukuru kwa yote aliyokutendea?