Date: 
26-02-2021
Reading: 
Luke 22:40-46

FRIDAY 26TH FEBRUARY 2021 MORNING                                                      

Luke 22:40-46 New International Version (NIV)

40 On reaching the place, he said to them, “Pray that you will not fall into temptation.” 41 He withdrew about a stone’s throw beyond them, knelt down and prayed, 42 “Father, if you are willing, take this cup from me; yet not my will, but yours be done.” 43 An angel from heaven appeared to him and strengthened him. 44 And being in anguish, he prayed more earnestly, and his sweat was like drops of blood falling to the ground.[c]

45 When he rose from prayer and went back to the disciples, he found them asleep, exhausted from sorrow. 46 “Why are you sleeping?” he asked them. “Get up and pray so that you will not fall into temptation.”

The human race originally fell into temptation and sin in a garden. Jesus, resisted temptation and overcame the enemy in the garden of Gethsemane. If we want to overcome the trials and temptations that hit us, we must learn from our Lord how to pray as He prayed. “If He prayed who was without sin, how much more it becomes a sinner to pray. So the options are: prayer or temptation.


IJUMAA TAREHE 26 FEBRUARI 2021  ASUBUHI                                      

LUKA 22:40-46

40 Alipofika mahali pale aliwaambia, Ombeni kwamba msiingie majaribuni.
41 Mwenyewe akajitenga nao kama kiasi cha kutupa jiwe, akapiga magoti akaomba,
42 akisema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke.
43 Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu.
44 Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba; hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini.]
45 Alipoondoka katika kuomba kwake, akawajia wanafunzi wake, akawakuta wamelala usingizi kwa huzuni.
46 Akawaambia, Mbona mmelala usingizi? Ondokeni, mkaombe, msije mkaingia majaribuni.

Mwanadamu katika mwanzo wa maisha yake alianguka katika majaribu na kutenda dhambi katika bustani ya Edeni. Yesu aliyapinga majaribu na kumshinda adui katika bustani ya Gethsemane. Ikiwa tunataka kushinda majaribu yanayotushambulia, ni lazima tujifunze kutoka kwa Bwana wetu Yesu Kristo namna ya kuomba kama yeye alivyoomba. Ikiwa yeye asiyekuwa na dhambi aliomba, je, sisi wenye dhambi tunapaswa kuomba kwa namna gani? Hivyo basi, tunao uchaguzi; kudumu katika maombi au kuanguka katika majaribu.