Date: 
21-10-2022
Reading: 
Luka 4:30-31

Ijumaa asubuhi tarehe 21.10.2022

Luka 4:31-37

[31]

Akashuka mpaka Kapernaumu, mji wa Galilaya, akawa akiwafundisha siku ya sabato;

[32]wakashangaa mno kwa mafundisho yake, kwa kuwa neno lake lilikuwa na uwezo.

[33]Na ndani ya sinagogi mlikuwa na mtu mwenye roho ya pepo mchafu, akalia kwa sauti kuu,

[34]akisema, Acha! Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Umekuja kutuangamiza? Nakujua u nani, Mtakatifu wa Mungu.

[35]Yesu akamkemea, akisema, Fumba kinywa, mtoke. Ndipo yule pepo akamwangusha katikati, akamtoka asimdhuru neno.

[36]Mshangao ukawashika wote, wakasemezana wakisema, Ni neno gani hili, maana awaamuru pepo wachafu kwa uwezo na nguvu, nao hutoka.

[37]Habari zake zikaenea kila mahali katika nchi ile.

Upendo wa kweli watoka kwa Mungu;

Yesu yuko Kapernaumu akihubiri siku ya sabato. Katikati ya mahubiri anatokea mtu mwenye pepo mchafu, na Yesu anamkemea pepo mchafu anamtoka. Wengi walishangaa uwezo wake wa kuhubiri na kufundisha, lakini zaidi jinsi alivyotoa pepo.

Yesu alikatisha mahubiri yake kumponya mwenye pepo. Hakuona haja ya kuendelea kuhubiri wakati kuna mwenye pepo anateseka. Mungu hakuwa tayari tukae dhambini ndiyo maana alimtuma Yesu afe msalabani kwa ajili yetu. Yesu yuko tayari kutuponya na kututunza. Tumwendee kwa Imani maana upendo wa kweli watoka kwake. Siku njema.