Date: 
30-03-2021
Reading: 
Luka 22:7-13

JUMANNE TAREHE 30 MACHI 2021, ASUBUHI

Luka 22:7-13 Neno: Bibilia Takatifu

Ikafika siku ya Mikate isiyotiwa Chachu. Siku hiyo Mwana- Kondoo wa Pasaka huchinjwa. Yesu akawatuma Petro na Yohana, akawaagiza, “Nendeni mkatuandalie chakula cha Pasaka.” Wakam wuliza, “Tukaandae wapi?” 10 Akawajibu, “Mtakapokuwa mnaingia mjini, mtakutana na mwanaume aliyebeba mtungi wa maji. Mfuateni mpaka kwenye nyumba atakayoingia, 11 kisha mwambieni mwenye nyumba, Mwalimu anauliza, kiko wapi chumba cha wageni, ambamo mimi na wanafunzi wangu tutakula Pasaka? 12 Atawaonyesha chumba kikubwa ghorofani ambacho kina fanicha zote. Fanyeni maandalizi humo.”

13 Wakaenda wakakuta kila kitu kama Yesu alivyokuwa amewaambia. Kwa hiyo wakaandaa chakula cha Pasaka.

Read full chapter

Yesu anaingia Yerusalemu kwa shangwe;

Yesu anawatuma Petro na Yohana kwenda kumuandalia Pasaka. Wanaenda hadi kwenye nyumba aliyowaelekeza, wanafanya vile vile alivyowaambia, yaani kuandaa sehemu ya kulia Pasaka.

Baadae anaketi nao chakulani akiadhimisha karamu Takatifu. Maandalizi haya  yalikuwa ni kuwakumbusha wanafunzi kuwa Pasaka inakaribia, hivyo kujiandaa kusherehekea.

Pasaka ya wakati ule walisherehekea kukombolewa utumwani. Pasaka ya leo tunakumbuka Yesu alivyotukomboa kwa njia ya kifo msalabani. Tunakumbuka Yesu alivyo mwana kondoo wa Pasaka.

Yesu Yesu aliwaandaa wanafunzi kuila Pasaka. Sisi tumejiandaaje kusherehekea Pasaka? Tunapojiandaa kukumbuka jinsi tulivyokombolewa, tutafakari njia zetu, ili kwa kifo chake tupate uzima wa milele.

Siku njema.


MONDAY 30TH MARCH 2021, MORNING

Luke 22:7-13, New International Version

The Last Supper

Then came the day of Unleavened Bread on which the Passover lamb had to be sacrificed. Jesus sent Peter and John, saying, “Go and make preparations for us to eat the Passover.”

“Where do you want us to prepare for it?” they asked.

10 He replied, “As you enter the city, a man carrying a jar of water will meet you. Follow him to the house that he enters, 11 and say to the owner of the house, ‘The Teacher asks: Where is the guest room, where I may eat the Passover with my disciples?’ 12 He will show you a large room upstairs, all furnished. Make preparations there.”

13 They left and found things just as Jesus had told them. So they prepared the Passover.

Read full chapter

Jesus enters Jerusalem with joy;

Jesus sends Peter and John to prepare the Passover meal for him. They go to the house that he has directed to them, and they do exactly as he has told them, namely, to prepare the place for the Passover.

Later he sits down to eat with them, celebrating the Lord's Supper. This preparation was to remind students that the Passover was approaching, so prepare to celebrate.

The Passover of that time celebrated the deliverance from bondage. Today's Passover we remember how Jesus redeemed us through death on the cross. We remember Jesus being the Passover lamb.

Jesus prepared the disciples for the Passover meal. How are we prepared to celebrate Easter? As we prepare to remember how we have been redeemed, we will reflect on our ways, so that by his death we may have eternal life.

Good day.