Date: 
27-03-2021
Reading: 
Leviticus 16:15-22 (Walawi 16:15-22)

SATURDAY 27TH MARCH 2021     MORNING                                                      

Leviticus 16:15-22  New International Version (NIV)

15 “He shall then slaughter the goat for the sin offering for the people and take its blood behind the curtain and do with it as he did with the bull’s blood: He shall sprinkle it on the atonement cover and in front of it. 16 In this way he will make atonement for the Most Holy Place because of the uncleanness and rebellion of the Israelites, whatever their sins have been. He is to do the same for the tent of meeting, which is among them in the midst of their uncleanness. 17 No one is to be in the tent of meeting from the time Aaron goes in to make atonement in the Most Holy Place until he comes out, having made atonement for himself, his household and the whole community of Israel.

18 “Then he shall come out to the altar that is before the Lord and make atonement for it. He shall take some of the bull’s blood and some of the goat’s blood and put it on all the horns of the altar. 19 He shall sprinkle some of the blood on it with his finger seven times to cleanse it and to consecrate it from the uncleanness of the Israelites.

20 “When Aaron has finished making atonement for the Most Holy Place, the tent of meeting and the altar, he shall bring forward the live goat. 21 He is to lay both hands on the head of the live goat and confess over it all the wickedness and rebellion of the Israelites—all their sins—and put them on the goat’s head. He shall send the goat away into the wilderness in the care of someone appointed for the task. 22 The goat will carry on itself all their sins to a remote place; and the man shall release it in the wilderness.

We can only come into God’s Holy Place at His invitation. Blessedly, the access has been opened wide because of Jesus’ work on the cross for us. Romans 5:1-2 specifically says that, because of Jesus’ work on our behalf, we have standing access to God.


JUMAMOSI  TAREHE 27 MACHI 2021      ASUBUHI                                         

WALAWI 16:15-22

15 Kisha atamchinja yule mbuzi wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya watu, na kuileta damu yake ndani ya pazia, na kwa damu hiyo atafanya vile vile kama alivyofanya kwa damu ya ng'ombe, na kuinyunyiza juu ya kiti cha rehema, na mbele ya kiti cha rehema,
16 naye atafanya upatanisho kwa ajili ya mahali patakatifu, kwa sababu ya mambo machafu ya wana wa Israeli, na kwa sababu ya makosa yao, naam, kwa ajili ya dhambi zao zote; naye atafanya vile vile kwa ajili ya hema ya kukutania, ikaayo pamoja nao katikati ya machafu yao.
17 Wala hapatakuwa na mtu katika hema ya kukutania, wakati aingiapo ili kufanya upatanisho katika patakatifu, hata atakapotoka nje, baada ya kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, na kwa ajili ya nyumba yake, na kwa ajili ya mkutano wote wa Israeli.
18 Kisha atatoka na kuiendea madhabahu iliyo mbele za Bwana na kufanya upatanisho kwa ajili yake; atatwaa baadhi ya damu ya yule ng'ombe, na ya damu ya yule mbuzi, na kuitia juu ya pembe za madhabahu pande zote.
19 Tena atanyunyiza baadhi ya damu juu ya madhabahu kwa kidole chake mara saba, na kuitakasa, ili machafu yote ya wana wa Israeli yaitoke.
20 Naye akiisha kufanya upatanisho kwa ajili ya mahali patakatifu, na hema ya kukutania, na madhabahu, atamleta yule mbuzi aliye hai.
21 Na Haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha yule mbuzi aliye hai, na kuungama juu yake uovu wote wa wana wa Israeli, na makosa yao, naam, dhambi zao zote; naye ataziweka juu ya kichwa chake yule mbuzi, kisha atampeleka aende jangwani kwa mkono wa mtu aliye tayari.
22 Na yule mbuzi atachukua juu yake uovu wao wote, mpaka nchi isiyo watu; naye atamwacha mbuzi jangwani.

Tunaweza kukaribia mahali patakatifu pa Mungu kwa mwaliko wake mwenyewe. Tunayo heri, maana njia imewekwa wazi kwa sababu ya kazi ya Yesu pale msalabani kwa ajili yetu. Warumi 5:1-2 inasema kwa kina kuwa, kwa sababu ya kazi ya Yesu aliyofanya badala yetu, tunayo ruhusa ya kumkaribia Mungu.