Date: 
23-03-2021
Reading: 
Leviticus 16:1-14 ( Walawi 16:1-14)

TUESDAY 23RD MARCH 2021    MORNING                                 

Leviticus 16:1-14 New International Version (NIV)

16 The Lord spoke to Moses after the death of the two sons of Aaron who died when they approached the Lord. The Lord said to Moses: “Tell your brother Aaron that he is not to come whenever he chooses into the Most Holy Place behind the curtain in front of the atonement cover on the ark, or else he will die. For I will appear in the cloud over the atonement cover.

“This is how Aaron is to enter the Most Holy Place: He must first bring a young bull for a sin offering[a] and a ram for a burnt offering. He is to put on the sacred linen tunic, with linen undergarments next to his body; he is to tie the linen sash around him and put on the linen turban. These are sacred garments; so he must bathe himself with water before he puts them on. From the Israelite community he is to take two male goats for a sin offering and a ram for a burnt offering.

“Aaron is to offer the bull for his own sin offering to make atonement for himself and his household. Then he is to take the two goats and present them before the Lord at the entrance to the tent of meeting. He is to cast lots for the two goats—one lot for the Lord and the other for the scapegoat.[b] Aaron shall bring the goat whose lot falls to the Lord and sacrifice it for a sin offering. 10 But the goat chosen by lot as the scapegoat shall be presented alive before the Lord to be used for making atonement by sending it into the wilderness as a scapegoat.

11 “Aaron shall bring the bull for his own sin offering to make atonement for himself and his household, and he is to slaughter the bull for his own sin offering. 12 He is to take a censer full of burning coals from the altar before the Lord and two handfuls of finely ground fragrant incense and take them behind the curtain. 13 He is to put the incense on the fire before the Lord, and the smoke of the incense will conceal the atonement cover above the tablets of the covenant law, so that he will not die. 14 He is to take some of the bull’s blood and with his finger sprinkle it on the front of the atonement cover; then he shall sprinkle some of it with his finger seven times before the atonement cover.

Jesus has forgiven our sins, and reconciled us to Himself.  He invites you to trust Him for that work of atonement. Is your life marked by the “confidence” and “assurance” to “enter the holy places”, every day? God calls us to come in prayer, with confession, with petition, with joy; to come before His throne and to value his glory; to enjoy its warmth and light.


JUMANNE TAREHE 23 MARCH 2021     ASUBUHI                    

MAMBO YA WALAWI 16:1-14

1 Bwana akasema na Musa, baada ya kufa kwa hao wana wawili wa Haruni, walipokaribia mbele za Bwana, wakafa;
Bwana akamwambia Musa, Sema na Haruni ndugu yako, kwamba asiingie wakati wo wote katika mahali patakatifu ndani ya pazia, mbele ya kiti cha rehema, kilicho juu ya sanduku, asije akafa; maana, mimi nitaonekana katika lile wingu juu ya kiti cha rehema.
Haruni ataingia katika patakatifu na vitu hivi; ng'ombe mume mchanga kwa sadaka ya dhambi, na kondoo mume kwa sadaka ya kuteketezwa.
Ataivaa ile kanzu takatifu ya kitani, atakuwa na zile suruali za kitani mwilini mwake, atafungwa ule mshipi wa kitani, naye atavaa ile kofia ya kitani; hayo ndiyo mavazi matakatifu, naye ataoga mwili wake majini, na kuyavaa.
Kisha atatwaa mikononi mwa mkutano wa Waisraeli mbuzi waume wawili, kwa sadaka ya dhambi; na kondoo mume kwa sadaka ya kuteketezwa.
Na Haruni atamtoa yule ng'ombe wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya nafsi yake, na kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, na kwa ajili ya nyumba yake.
Kisha atawatwaa wale mbuzi wawili na kuwaweka mbele za Bwana mlangoni pa hema ya kukutania.
Na Haruni atapiga kura juu ya wale mbuzi wawili; kura moja kwa ajili ya Bwana; na kura ya pili kwa ajili ya Azazeli.
Na Haruni atamleta yule mbuzi aliyeangukiwa na kura kwa ajili ya Bwana, na kumtoa awe sadaka ya dhambi.
10 Bali yule mbuzi aliyeangukiwa na kura kwa ajili ya Azazeli atawekwa hai mbele za Bwana ili kumfanyia upatanisho, ili kumpeleka jangwani kwa ajili ya Azazeli.
11 Na Haruni atamsongeza ng'ombe wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya nafsi yake, na kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, na kwa ajili ya nyumba yake; naye atamchinja yule ng'ombe wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya nafsi yake.
12 Kisha atatwaa chetezo kilichojaa makaa ya moto yatokayo katika madhabahu iliyo mbele za Bwana, na konzi mbili za uvumba mzuri uliopondwa sana, mikononi mwake, naye atauleta ndani ya pazia.
13 Kisha atatia ule uvumba juu ya moto mbele za Bwana, ili moshi wa ule uvumba ukisitiri kiti cha rehema kilicho juu ya ushuhuda, asije akafa.
14 Kisha atatwaa baadhi ya damu ya yule ng'ombe, na kuinyunyiza kwa kidole chake juu ya kiti cha rehema upande wa mashariki; na mbele ya kiti cha rehema atainyunyiza ile damu kwa kidole chake mara saba.

Yesu ametusamehe dhambi zetu, na ametupatanisha kwake mwenyewe. Anakukaribisha kuamini katika kazi hii ya upatanisho aliyoifanya. Je, maisha yako yana alama ya “ujasiri” na “uhakika” wa “kuingia mahali patakatifu” kila siku? Mungu anatukaribisha kwenda mbele zake kwa maombi, kwa njia ya toba, maombezi, kwa Furaha; twende mbele ya kiti chake cha enzi kwa kuheshimu utukufu wake; na kufurahia upendo na nuru yake.