Date: 
13-12-2022
Reading: 
Kumbukumbu la Torati 18:15-22

Hii ni Advent 

Jumanne asubuhi tarehe 13.12.2022

Kumbukumbu la Torati 18:15-22

[15]BWANA, Mungu wako, atakuondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zako kama nilivyo mimi; msikilizeni yeye.

[16]Kama vile ulivyotaka kwa BWANA, Mungu wako, huko Horebu, siku ya kusanyiko, ukisema, Nisisikie tena sauti ya BWANA, Mungu wangu, wala nisiuone tena moto huu mkubwa, nisije nikafa.

[17]BWANA akaniambia, Wametenda vema kusema walivyosema.

[18]Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru.

[19]Hata itakuwa, mtu asiyesikiliza maneno yangu atakayosema yule kwa jina langu, nitalitaka kwake.

[20]Lakini nabii atakayenena neno kwa kujikinai kwa jina langu, ambalo sikumwagiza kulinena, au atakayenena katika jina la miungu mingine, nabii yule atakufa.

[21]Nawe ukisema moyoni mwako, Tutajuaje neno asilolinena BWANA?

[22]Atakaponena nabii kwa jina la BWANA, lisifuate jambo lile wala kutimia, hilo ndilo neno asilolinena BWANA; kwa kujikinai amelinena huyo nabii, usimwogope

Bwana anawafariji watu wake;

Katika Torati tunayoisoma asubuhi hii, Bwana anawaambia Israeli kwamba asingewapungukia, na katika kuhakikisha wanadumu katika Agano lake, anawaahidi kuwapa Nabii kama alivyokuwa Musa ambaye atawaambia yote atakayowaamuru. Bwana anawasisitizia watu wake kumsikiliza Nabii wake, maana atanena neno lake.

Ahadi hii ya Mungu inaishi kwetu hadi leo. Mungu alimtuma mwana wake wa pekee Yesu Kristo atukomboe kwa njia ya kifo msalabani. Huyu ndiye mwenye faraja ya kweli, tunayekumbushwa kusikia habari zake na kumpokea kwa ajili ya uzima wetu, sasa na hata milele.

Siku njema.