Date: 
03-07-2018
Reading: 
Judges 6:22-32 (Waamuzi 6:22-32)

TUESDAY 3rd  JULY 2018  MORNING                                               

Judges 6:22-32 New International Version (NIV)

22 When Gideon realized that it was the angel of the Lord, he exclaimed, “Alas, Sovereign Lord! I have seen the angel of the Lord face to face!”

23 But the Lord said to him, “Peace! Do not be afraid. You are not going to die.”

24 So Gideon built an altar to the Lord there and called it The Lord Is Peace. To this day it stands in Ophrah of the Abiezrites.

25 That same night the Lord said to him, “Take the second bull from your father’s herd, the one seven years old.[a] Tear down your father’s altar to Baal and cut down the Asherah pole[b] beside it. 26 Then build a proper kind of[c] altar to the Lord your God on the top of this height. Using the wood of the Asherah pole that you cut down, offer the second[d] bull as a burnt offering.”

27 So Gideon took ten of his servants and did as the Lord told him. But because he was afraid of his family and the townspeople, he did it at night rather than in the daytime.

28 In the morning when the people of the town got up, there was Baal’s altar, demolished, with the Asherah pole beside it cut down and the second bull sacrificed on the newly built altar!

29 They asked each other, “Who did this?”

When they carefully investigated, they were told, “Gideon son of Joash did it.”

30 The people of the town demanded of Joash, “Bring out your son. He must die, because he has broken down Baal’s altar and cut down the Asherah pole beside it.”

31 But Joash replied to the hostile crowd around him, “Are you going to plead Baal’s cause? Are you trying to save him? Whoever fights for him shall be put to death by morning! If Baal really is a god, he can defend himself when someone breaks down his altar.” 32 So because Gideon broke down Baal’s altar, they gave him the name Jerub-Baal[e] that day, saying, “Let Baal contend with him.”

Footnotes:

  • Judges 6:25 Or Take a full-grown, mature bull from your father’s herd
  • Judges 6:25 That is, a wooden symbol of the goddess Asherah; also in verses 26, 28 and 30
  • Judges 6:26 Or build with layers of stone an
  • Judges 6:26 Or full-grown; also in verse 28
  • Judges 6:32 Jerub-Baal probably means let Baal contend.

Gideon obeyed God. He destroyed the altars to false gods and built and altar to the true God. Then Gideon offered sacrifices to God. The people were angry but Gideon’s father stood up for him.

Let us stand up for the truth. Let us worship the true God and not be intimidated by what other people think. 

 

JUMANNE TAREHE 3 JUALI 2018 ASUBUHI                               

WAAMUZI 6:22-32

22 Gideoni akaona ya kuwa ni malaika wa Bwana; Gideoni akasema, Ole wangu, Ee Bwana MUNGU! Kwa kuwa nimemwona Bwana uso kwa uso. 
23 Bwana akamwambia Amani iwe pamoja nawe; usiogope; hutakufa. 
24 Ndipo Gideoni akamjengea Bwana madhabahu hapo, akaiita jina lake, Yehova-Shalomu; hata hivi leo iko huko katika Ofra ya Waabiezeri. 
25 Ikawa usiku uo huo Bwana akamwambia, Mtwae ng'ombe wa baba yako, yaani ng'ombe wa pili, wa miaka saba, ukaiangushe madhabahu ya Baali, aliyo nayo baba yako, ukaikate Ashera ile iliyo karibu nayo; 
26 ukamjengee Bwana, Mungu wako, madhabahu juu ya ngome hii, kwa taratibu zake; ukamtwae yule ng'ombe wa pili na kumtoa awe sadaka ya kuteketezwa, kwa kuni za ile Ashera uliyoikata. 
27 Ndipo Gideoni akatwaa watu kumi miongoni mwa watumishi wake, akafanya kama Bwana alivyomwambia; lakini ikawa kwa sababu aliwaogopa watu wa nyumba ya baba yake, na watu wa mji, hakuweza kuyatenda hayo wakati wa mchana, basi aliyatenda usiku. 
28 Hata watu wa mji walipoondoka asubuhi na mapema, tazama, madhabahu ya Baali imebomolewa, na ile Ashera iliyokuwa karibu nayo imekatwa, na yule ng'ombe wa pili ametolewa sadaka juu ya ile madhabahu iliyojengwa. 
29 Wakaambiana, Ni nani aliyetenda jambo hili? Hata walipotafuta habari na kuuliza, wakasema, Gideoni, mwana wa Yoashi, ndiye aliyetenda jambo hili. 
30 Ndipo watu wa mji wakamwambia Yoashi Mlete mwanao, afe; kwa sababu ameibomoa madhabahu ya Baali na kwa sababu ameikata ile Ashera iliyokuwa karibu nayo. 
31 Yoashi akawaambia watu wote waliokuwa wakishindana naye, Je! Mtamtetea Baali? Au mtamwokoa ninyi? Yeye atakayemtetea na auawe hivi asubuhi; kama yeye ni Mungu, na ajitetee nafsi yake, kwa sababu mtu mmoja ameibomoa madhabahu yake. 
32 Basi akamwita Yerubaali siku hiyo, akisema, Baali na atete naye kwa ajili ya nafsi yake, kwa sababu ameibomoa madhabahu yake. 
 

Gideoni alifanya uamuzi vyema. Alivunja madhabahu ya miungu ya wongo. Halafu alijenga madhabahu kwa Mungu wa kweli na alichinja sadaka ya ng’ombe dume kwa ajili ya Bwana. Watu walikasirikia matendo ya Gideoni lakini baba yake alimtetea.

Tufanye uamuzi mema na kumwabudu Mungu wa kweli. Tusiogope mawazo ya watu. Mungu atusaidie tuwe na ujasiri.