Date: 
08-12-2022
Reading: 
Isaya 28:20-22

Hii ni Advent 

Alhamisi asubuhi tarehe 08.12.2022

Isaya 28:20-22

20 Maana kitanda kile ni kifupi asiweze mtu kujinyosha juu yake, na nguo ile ya kujifunika ni nyembamba asipate mtu kujizingisha.

21 Maana Bwana ataondoka kama vile katika mlima Perasimu, ataghadhibika kama vile katika bonde la Gibeoni; apate kufanya kazi yake, kazi yake ya ajabu; na kulitimiza tendo lake, tendo lake la ajabu.

22 Basi sasa msiwe watu wenye kudharau, vifungo vyenu msije vikakazwa; maana nimesikia kwa Bwana, Bwana wa majeshi, habari ya hukumu itakayotimizwa, nayo imekusudiwa, itakayoipata dunia yote pia.

Bwana anakuja tuandae mioyo yetu;

Nabii Isaya anaonesha ghadhabu ya Mungu kwa watu wasiomwamini na kumfuata. Ni katika kuwaokoa, Mungu anawaagiza watu wake kutodharau na kuacha ujumbe wa Bwana ulioletwa kwao. Ujumbe huu walipewa Israeli kabla ya kwenda uhamishoni Babeli.

Tunapokumbushwa kurudi kwa Kristo kwa mara ya pili, tusiudharau na kuuacha ujumbe wa Bwana unaoletwa kwetu na watumishi wake. Neno la Mungu lituongoze kudumu katika imani tunapongojea kurudi kwake kwa mara ya pili.

Uwe na siku njema.