Date: 
06-03-2018
Reading: 
Isaiah 49:22-26 (Isaya 49:22-26)

TUESDAY 6TH MARCH 2018 MORNING                                 

Isaiah 49:22-26 New International Version (NIV)

22 This is what the Sovereign Lord says:

“See, I will beckon to the nations,
    I will lift up my banner to the peoples;
they will bring your sons in their arms

    and carry your daughters on their hips.
23 Kings will be your foster fathers,
    and their queens your nursing mothers.
They will bow down before you with their faces to the ground;

    they will lick the dust at your feet.
Then you will know that I am the Lord;

    those who hope in me will not be disappointed.”

24 Can plunder be taken from warriors,
    or captives be rescued from the fierce[a]?

25 But this is what the Lord says:

“Yes, captives will be taken from warriors,
    and plunder retrieved from the fierce;
I will contend with those who contend with you,

    and your children I will save.
26 I will make your oppressors eat their own flesh;
    they will be drunk on their own blood, as with wine.
Then all mankind will know

    that I, the Lord, am your Savior,
    your Redeemer, the Mighty One of Jacob.”

Footnotes:

  1. Isaiah 49:24 Dead Sea Scrolls, Vulgate and Syriac (see also Septuagint and verse 25); Masoretic Text righteous

 

These are words of comfort and hope. God promises to restore and bless His people Israel. The former enemies will honour God and His people.

When we honour and obey God He will lift us up and we will be respected.  Let us thank God for His wonderful promises to us and let us always obey Him and put Him first in our lives.

 

JUMANNE TAREHE 6 MACHI 2018 ASUBUHI                              

ISAYA  49:22-26

22 Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, nitawainulia mataifa mkono wangu, na kuwatwekea kabila za watu bendera yangu; nao wataleta wana wako vifuani mwao, na binti zako watachukuliwa mabegani mwao. 
23 Na wafalme watakuwa baba zako za kulea, na malkia zao mama zako za kulea; watainama mbele yako kifudifudi, na kuramba mavumbi ya miguu yako; nawe utajua ya kuwa mimi ni Bwana, tena waningojeao hawatatahayarika. 
24 Je! Aliye hodari aweza kunyang'anywa mateka yake, au jeshi lao waliofungwa halali wataokoka? 
25 Naam, Bwana asema hivi, Hata jeshi la wafungwa wake aliye hodari watapokonywa mikononi mwake, na mateka yake aliye jabari wataokoka; kwa maana nitateta na yeye atetaye nawe, nami nitawaletea wana wako wokovu. 
26 Na hao wanaokuonea nitawalisha nyama yao wenyewe, nao watalewa kwa kuinywa damu yao wenyewe, kama kwa mvinyo mpya; na wote wenye mwili watajua ya kuwa mimi, Bwana, ni mwokozi wako, na Mkombozi wako ni Mwenye enzi wa Yakobo.

Maneno haya juu ni maneno ya faraja na tumaini. Mungu aliahidi kubariki na kuinua taifa lake Israeli. Hata mataifa mengine ambao walikuwa maadui zao watabadilika na kuanza kumheshimu Mungu na taifa lake Israeli.

Tumtukuze na tumtii Mungu na yeye atatuinua na kutubariki.