Date: 
16-04-2021
Reading: 
Hesabu 12:6-8 (Numbers 12:6-8)

JUMATANO TAREHE 16 APRILI 2021, ASUBUHI

Hesabu 12:6-8

6 Kisha Mwenyezi-Mungu akawaambia, “Sikilizeni maneno yangu: Kama kuna nabii miongoni mwenu, mimi Mwenyezi-Mungu hujifahamisha kwake katika maono na kuongea naye katika ndoto. 7 Lakini kumhusu mtumishi wangu Musa, hali ni tofauti kabisa. Yeye ana jukumu la kuwatunza watu wangu wote. 8 Mimi huongea naye ana kwa ana, waziwazi na si kwa kutumia mafumbo. Yeye huliona umbo langu mimi Mwenyezi-Mungu. Kwa nini, basi, hamkuogopa kusema vibaya dhidi ya mtumishi wangu Musa?”

Musa alimuoa mwanamke Mkushi, Miriamu na Haruni wakamuonea wivu na kumnenea vibaya. Mungu anawatokea Miriamu na Haruni na kuwaambia maneno tuliyoyasoma hapo juu.

Ukisoma zaidi, unaona kuwa baadae  Miriamu alipata ugonjwa wa ukoma! Haruni akaomba toba huku Musa akiomba uponyaji wa Miriamu.

Funzo;

Miriamu na Haruni walimnenea Musa  isivyofaa.

Hili ni jambo la kutafakari sana, kama sisi wenyewe tunapendana na kuneneana mema. Maneno huonyesha hisia zetu, yaani jinsi tunavyowaza juu ya wengine. Ni wakati wa kufikiria tunavyowaza juu ya wengine.

Kwa tafsiri pana ni mtazamo juu ya wenzetu. Tujihoji; sisi ni mfano wa Yesu katika kuwawazia wenzetu mema? Sisi tunawapenda wenzetu? Kuwapenda wenzetu ni agizo, vinginevyo hukumu ya Mungu inatungoja. Ijumaa njema.


WEDNESDAY 16TH APRIL 2021, MORNING

Numbers 12:6-8

He said, “Listen to my words:

“When there is a prophet among you,
    I, the Lord, reveal myself to them in visions,
    I speak to them in dreams.
But this is not true of my servant Moses;
    he is faithful in all my house.
With him I speak face to face,
    clearly and not in riddles;
    he sees the form of the Lord.
Why then were you not afraid
    to speak against my servant Moses?”

Read full chapter

Moses married a Cushite woman, and Miriam and Aaron became jealous of him and spoke abusively of him. God appears to Miriam and Aaron and tells them the words we read in the above text.

If you read further in this chapter, you will see that Miriam later contracted leprosy! Aaron prayed for repentance while Moses prayed for Miriam's healing.

Lesson;

Miriam and Aaron spoke against Moses.

This is a very serious matter, as we love one another and speak well of one another. Words express our feelings, that is, how we think about others. It's time reflect on how we think, talk, about others.

In a broader sense it is a view of our peers. Let's ask ourselves; Are we imitating Jesus in showing consideration for others? Do we love our neighbour? Loving others is a command; otherwise God's judgment awaits us. Have a Good Friday.