SATURDAY 16TH JANUARY 2021 MORNING
Hebrews 6:1-8 New International Version (NIV)
Therefore let us move beyond the elementary teachings about Christ and be taken forward to maturity, not laying again the foundation of repentance from acts that lead to death,[a] and of faith in God, 2 instruction about cleansing rites,[b] the laying on of hands, the resurrection of the dead, and eternal judgment. 3 And God permitting, we will do so.
4 It is impossible for those who have once been enlightened, who have tasted the heavenly gift, who have shared in the Holy Spirit, 5 who have tasted the goodness of the word of God and the powers of the coming age 6 and who have fallen[c] away, to be brought back to repentance. To their loss they are crucifying the Son of God all over again and subjecting him to public disgrace. 7 Land that drinks in the rain often falling on it and that produces a crop useful to those for whom it is farmed receives the blessing of God. 8 But land that produces thorns and thistles is worthless and is in danger of being cursed. In the end it will be burned.
The scripture clearly teaches that God is the one who saves and He alone grants repentance. He alone opens hearts to believe and He alone keeps His children. Only God grants true assurance to His children.
I pray that we all are in the process of moving on to maturity through the Spirit’s work.
JUMAMOSI TAREHE 16 JANUARI 2021 ASUBUHI WAEBRANIA 6:1-8
Kwa sababu hiyo, tukiacha kuyanena mafundisho ya kwanza ya Kristo, tukaze mwendo ili tuufikilie utimilifu; tusiweke msingi tena wa kuzitubia kazi zisizo na uhai, na wa kuwa na imani kwa Mungu,
2 na wa mafundisho ya mabatizo, na kuwekea mikono, na kufufuliwa wafu, na hukumu ya milele.
3 Na hayo tutafanya Mungu akitujalia.
4 Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu,
5 na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo,
6 wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.
7 Maana nchi inayoinywa mvua inayoinyeshea mara kwa mara, na kuzaa mboga zenye manufaa kwa hao ambao kwa ajili yao yalimwa, hushiriki baraka zitokazo kwa Mungu;
8 bali ikitoa miiba na magugu hukataliwa na kuwa karibu na laana; ambayo mwisho wake ni kuteketezwa.
Maandiko yanatufundisha wazi kwamba Mungu pekee ndiye aokoaye na ndiye pekee mwenye kusamehe dhambi. Yeye pekee hufungua mioyo ili tuweze kumwamini na ndiye anayewatunza watoto wake na kuwapa hakika ya wokovu. Ni ombi langu kuwa sisi sote tunakaza mwendo ili kufikia ule utimilifu kwa njia ya Roho Mtakatifu.