Date: 
13-02-2018
Reading: 
Hebrews 13:10-16 NIV (Waebrania 13:10-16)

TUESDAY 13TH FEBRUARY 2018 MORNING                   HEBREWS 13:10-16

Hebrews 13:10-16 New International Version (NIV)

10 We have an altar from which those who minister at the tabernacle have no right to eat.

11 The high priest carries the blood of animals into the Most Holy Place as a sin offering, but the bodies are burned outside the camp. 12 And so Jesus also suffered outside the city gate to make the people holy through his own blood. 13 Let us, then, go to him outside the camp, bearing the disgrace he bore. 14 For here we do not have an enduring city, but we are looking for the city that is to come.

15 Through Jesus, therefore, let us continually offer to God a sacrifice of praise—the fruit of lips that openly profess his name. 16 And do not forget to do good and to share with others, for with such sacrifices God is pleased.

The Epistle to the Hebrews explains how the Old and New Testament are related.  The Jewish High priests offered animal sacrifices to atone for the sins of the people. Jesus Christ is both High Priest and Lamb of God who died once on the cross to atone for the sins of all people.

Let us indeed praise God for our salvation and do good to others.

 

JUMANNE TAREHE 13 FEBRUARI  2018 ASUBUHI                   

WAEBRANIA 13:10-16

10 Tuna madhabahu ambayo wale waihudumiao ile hema hawana ruhusa kula vitu vyake. 
11 Maana wanyama wale ambao damu yao huletwa ndani ya patakatifu na kuhani mkuu kwa ajili ya dhambi, viwiliwili vyao huteketezwa nje ya kambi. 
12 Kwa ajili hii Yesu naye, ili awatakase watu kwa damu yake mwenyewe, aliteswa nje ya lango. 
13 Basi na tutoke tumwendee nje ya kambi, tukichukua shutumu lake. 
14 Maana hapa hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao. 
15 Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamayo jina lake. 
16 Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu. 


Waraka kwa Waebrania unatuelezea uhusiano katika Agano la Kale na Agano Jipya. Makuhani wa Kiyahudi walimtolea Mungu sadaka za wanyama kuomba msamaha wa dhambi kwa ajili ya watu. Yesu Kristo ni Kuhani Mkuu na pia alijitoa msalabani kama Kondoo wa Mungu. Alikufa kwa ajili ya dhambi zetu ili tuweze kuokolewa.

Tumsifu Mungu kwa wokovu huu na tuishi maisha yanayompendeza  Mungu.