Date: 
05-05-2017
Reading: 
Ezekiel 34:27-31 New International Version

JESUS CHRIST IS THE GOOD SHEPHERD 

Ezekiel 34:27-31 (Mathew 7:9-11)

Ezekiel 34:27-31 New International Version (NIV)

27 The trees will yield their fruit and the ground will yield its crops; the people will be secure in their land. They will know that I am the Lord, when I break the bars of their yoke and rescue them from the hands of those who enslaved them. 28 They will no longer be plundered by the nations, nor will wild animals devour them. They will live in safety, and no one will make them afraid. 29 I will provide for them a land renowned for its crops, and they will no longer be victims of famine in the land or bear the scorn of the nations. 30 Then they will know that I, the Lord their God, am with them and that they, the Israelites, are my people, declares the Sovereign Lord. 31 You are my sheep, the sheep of my pasture, and I am your God, declares the Sovereign Lord.’”

Jesus is the good shepherd, the good shepherd who gives His life for his people. Through this Jesus wants to bring you into a new, stronger covenant relationship with Him. A relationship in which you no longer depend upon the natural, limited resources this world's wealth, but to look to Him and His supernatural provisions for your life. He wants you to draw all that you need from Him. It is His will that there be a continual flow of His promised blessings into your life.

We are now living in a time of restoration.....a time of abundance of the blessings that God promised would come with the establishment of the Kingdom of God that Jesus was preaching about (Mark 1:14-15).

If you are a reader of the Bible, you would have been on a journey through the Word to discover God's plan to prosper and bless His people who walk in a covenant relationship with Him (Eze 34:30). 

His desire is that you become one of His people so as to bless you. It is God's will to bless and prosper you. Through His provision in the New Covenant, Jesus has made it possible for you to go directly to the Father, ask whatever you need, in His name and you will receive it.

God blessed and prospered Israel with abundance under the Old Covenant, which was based upon the blood of bulls and goats. How much more will God prosper and bless us today under the New Covenant, which is sealed and made effective by the blood of Jesus. Under this covenant relationship, God is our Father, and we are His very own children and we have DIRECT ACCESS to Him. Christ made this possible through the offering of Himself as the supreme sacrifice. 

Jesus said; "....Whatsoever you ask the Father in my name, he will give it to you...ask and you shall receive, that your joy may be full" (John 16:23-24). 

What is your greatest need today?

At Mathew 7:9-11 Jesus compares our relationship with the Father to our earthly relationship to our own children. One of the greatest joy as a parent is to give to our children the very best of all the things they need and desire. 

Jesus is asking that if we know how to give good gifts to our children, how much more will our Father in heaven give good gifts to those that ask Him?

HOW MUCH MORE will your Heavenly Father supply your financial needs!

HOW MUCH MORE will your Heavenly Father bless and prosper you!

HOW MUCH MORE will your Heavenly Father meet every need in your life!

Know that, it is God's will to prosper you, and that you should know His promises and act upon them in faith, and also honour Him with your "substance". But also know that God is your source of supply, and therefore saturate your heart and mind with the Word and walk in obedience to it. Lastly, ask in faith and you will receive.

YESU KRISTO NI MCHUNGAJI MWEMA - ANATUTUNZA

Ezekiel 34:27-31 (Mat 7:9-11)

27 Na mti wa kondeni utazaa matunda yake, nayo ardhi itatoa mazao yake, nao watakuwa salama katika nchi yao; nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, nitakapovunja vifungo vya kongwa lao, na kuwaokoa katika mikono ya watu wale waliowatumikisha.
28 Hawatakuwa mateka ya makafiri tena, wala mnyama wa nchi hatawala; bali watakaa salama salimini, wala hapana mtu atakayewatia hofu.
29 Nami nitawainulia miche iwe sifa njema, wala hawataangamizwa kwa njaa katika nchi yao tena, wala hawatachukua tena aibu ya makafiri.
30 Nao watajua ya kuwa mimi, Bwana, Mungu wao, ni pamoja nao, na ya kuwa wao, nyumba ya Israeli, ni watu wangu, asema Bwana MUNGU.
31 Na ninyi, kondoo zangu, kondoo za malisho yangu, ni wanadamu, na mimi ni Mungu wenu, asema Bwana MUNGU.

Ni ukweli usiopingika kuwa Yesu ni mchungaji mwema, Mchungaji mwema anayeutoa uhai wake kwa ajili ya watu wake. 

Kwa hilo, Yesu ana nia ya kusimika na wewe mahusiano yaliyo imara naye. Mahusiano ambayo hayategemei nguvu zetu na uchumi wa ulimwengu huu, wala ujanja wa akili zetu. Ni mpango wa Mungu tuwe tunamhitaji na kumtegemea Yeye kwa kila kitu tunachohitaji. Na kwa msingi huo, baraka zimiminike kwa watu, bila kukoma. Tambia kuwa tumo katika kipindi cha mrejesho wa utukufu wa Mungu uliopotea kwetu, muda wa kupokea baraka ambayo Mungu aliziagiza kwa watu wanaoishi katika ufalme wake, ambayo Yesu aliupigia mbiu (Mk 1:14-15).

Kama u msomaji wa Biblia, utagundua kwamba kinachoelezwa humu ni mpango mzima wa Mungu kuwaneemesha wale wanaotembea kwa kulifuata Neno lake la uzima na la agano naye (Eze 34:30). Anachotaka ni kuwa na wewe uwe mmoja wa wale anaotaka kuwabariki, ili akubariki na wewe pia. Ni baraka iliyoje kutafutwa ili ubarikiwe! 

Ni mapenzi yake Mungu kwetu kutubariki na kutuneemesha sisi kupitia agano jipya ambalo Yesu aliingia ili tupate upendeleo wa kwenda moja kwa moja na kuomba tutakacho, katika mapenzi yake, tutapewa. 

Ikiwa Mungu aliwabariki na kuwaneemesha Wana-Israel chini ya agano la kale ambalo lilisimikwa kwa damu ya mafahali na ya mbuzi, ni kwa kiasi gani basi atatubarikia sisi ambayo tumo katika Agano Jipya lililosimikwa kwa damu yake mwenyewe?

Chini ya Agano hili, Mungu ni Baba yetu, wote tuaminio! Na sisi ni wanawe na tuna ruhusa ya kwenda kwake moja kwa moja bila kupitia kwa kuhani wala mchungaji. Yesu alilithibitisha hili kwa kujitoa mwenyewe kuwa kafara.

Katika Yn 16:23-24 Yesu alisema; "...Mkimwomba Baba neno lolote atawapa kwa Jina langu.....ombeni nanyi mtapata, furaha Yesu iwe timilifu.

Wewe una mahitaji gani siku ya leo?

Ukisoma Mat 7:9-11, Yesu analinganisha uhusiano wetu na Mungu, kama ule tulionao na watoto wetu. Mzazi hupenda kumpa mwanawe kitu chema. Yesu anauliza, Kama sisi tunajua kuwapa wana wetu kilicho , chema si zaidi sana Baba yetu wa Mbinguni atawapa mema wao wamwombao? 

NI KWA KIASI GANI ZAIDI anaweza kukupa mahitaji yako ya kifedha?

NI KWA KIASI GANI ZAIDI anaweza kukubariki na kukuneemesha?

NI KWA KIASI GANI ZAIDI kukupa haja yako yote ya maisha yako?

Tambua kuwa;

  • Ni mpango wa Mungu kukutajirisha

  • Uzijue ahadi za Mungu na kuzifuatilia kuzitenda kwa Imani

  • Mheshimu Mungu kwa matoleo yako,

  • Ujue kuwa ni Mungu pekee akuwezeshaye na kukupa mahitaji yako yote

  • Uujaze moyo wako na Neno lake la uzima na kulitenda ipasavyo, 

  • Kisha omba kwa imani naye Mungu atakupa.

Tafakari sana hili!