Date: 
31-10-2016
Reading: 
2 Timothy 1:8-14 New International Version (NIV)

MONDAY 31ST OCTOBER 2016 MORNING                                        

2 Timothy 1:8-14  New International Version (NIV)

So do not be ashamed of the testimony about our Lord or of me his prisoner. Rather, join with me in suffering for the gospel, by the power of God. He has saved us and called us to a holy life—not because of anything we have done but because of his own purpose and grace. This grace was given us in Christ Jesus before the beginning of time, 10 but it has now been revealed through the appearing of our Savior, Christ Jesus, who has destroyed death and has brought life and immortality to light through the gospel. 11 And of this gospel I was appointed a herald and an apostle and a teacher. 12 That is why I am suffering as I am. Yet this is no cause for shame, because I know whom I have believed, and am convinced that he is able to guard what I have entrusted to him until that day.

13 What you heard from me, keep as the pattern of sound teaching, with faith and love in Christ Jesus. 14 Guard the good deposit that was entrusted to you—guard it with the help of the Holy Spirit who lives in us.

This letter was written by the Apostle Paul to Timothy who was his spiritual son and a young Pastor. In this letter and in the First letter to Timothy Paul gives advice and encouragement to Timothy.  In the above words Paul speaks of his own testimony and ministry and encourages Timothy to be faithful to God and to the sound Christian teaching which he has heard from Paul.

Pray that you will be faithful in you service to Christ wherever He has placed you and that you will not be mislead by false teachings.

 

JUMATATU TAREHE 31 OKTOBA 2016 ASUBUHI                      

2 TIMOTHEO 1:8-14

 

8 Basi usiuonee haya ushuhuda wa Bwana wetu, wala usinionee haya mimi mfungwa wake, bali uvumilie mabaya pamoja nami kwa ajili ya Injili, kwa kadiri ya nguvu ya Mungu; 
9 ambaye alituokoa akatuita kwa mwito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu sisi, bali kwa kadiri ya makusudi yake yeye na neema yake. Neema hiyo tulipewa katika Kristo Yesu tangu milele, 
10 na sasa inadhihirishwa kwa kufunuliwa kwake Mwokozi wetu Kristo Yesu; aliyebatili mauti, na kuufunua uzima na kutokuharibika, kwa ile Injili; 
11 ambayo kwa ajili ya hiyo naliwekwa niwe mhubiri na mtume na mwalimu. 
12 Kwa sababu hiyo nimepatikana na mateso haya, wala sitahayari; kwa maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kwamba aweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hata siku ile. 
13 Shika kielelezo cha maneno yenye uzima uliyoyasikia kwangu, katika imani na upendo ulio katika Kristo Yesu. 
14 Ilinde ile amana nzuri kwa Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu. 
   

Mtume Paulo anamwandikia Timotheo mtoto wake wa kiroho na Mchungaji kijana. Paulo anamshauri katika huduma yake.  Paulo anatoa ushuhuda wake na anamsihi Timotheo awe mwaminifu na alinde mafundisho sahihi ya Neno la Mungu.

Mungu atuwezeshe sisi tuwe waaminifu pia katika wajibu wote tuliopewa na tusipotoshwe na mafundisho ya uongo.