Date: 
20-10-2022
Reading: 
1Yohana 4:11-12

Alhamisi asubuhi tarehe 20.10.2022

1 Yohana 4:11-12

[11]Wapenzi ikiwa Mungu alitupenda sisi hivi, imetupasa na sisi kupendana.

[12]Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu.

Upendo wa kweli watoka kwa Mungu;

Yohana anaandika kuwa yafaa kwa watu kupendana wao kwa wao, wakiiga mfano wa Mungu aliyewapenda kwanza. Hakuna aliyemuona Mungu, bali upendo wake hudhihirika jinsi alivyotuumba na kututunza hadi leo. Naye hukaa na watu wake akiwatunza na kuwapa mahitaji yao ya kila siku. Huu ndiyo upendo wa Mungu kwetu.

Yohana anatusihi kupendana kama Mungu alivyotupenda. Katika kusisitiza hili anasema;

1 Yohana 4:16

[16]Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake.

Tukiwa na upendo Mungu hukaa ndani yetu, nasi hukaa ndani yake. Hii ndiyo habari njema, kuwa upendo hutuweka kwa Mungu, pia hutuweka pamoja. Tupendane kama Mungu alivyotupenda.

Alhamisi njema.