Date: 
22-12-2022
Reading: 
1Petro 4:3-6

Hii ni Advent 

Alhamisi asubuhi tarehe 22.12.2022

1 Petro 4:3-6

3 Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali;

4 mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao katika ufisadi ule ule usio na kiasi, wakiwatukana.

5 Nao watatoa hesabu kwake yeye aliye tayari kuwahukumu walio hai na waliokufa.

6 Maana kwa ajili hiyo hata hao waliokufa walihubiriwa Injili, ili kwamba wahukumiwe katika mwili kama wahukumiwavyo wanadamu; bali wawe hai katika roho kama Mungu alivyo hai.

Bwana yu karibu;

Petro analiandikia Kanisa la Mungu kuacha uovu, akiita dhambi maisha ya zamani. Kwa maana hiyo Petro analitaka Kanisa kumtazama Bwana na kujiepusha na dhambi. Petro anaweka wazi kuwa kila mtu atatoa hesabu yake mbele ya Bwana ahukumuye. Na kila mmoja atahukumiwa kwa kadri ya matendo yake maana hakuna ambaye hakuhubiriwa Injili.

Ujumbe wa Petro Alhamisi ya leo unatukumbusha kuwa dhambi itatupeleka motoni. Dhambi itasababisha tuukose uzima wa milele. Ndiyo maana Petro anatusihi kujiepusha na dhambi. Tujitayarishe kumlaki Bwana tukitenda mema, tayari kuurithi uzima wa milele.

Bwana yu karibu.

Alhamisi njema.