Date: 
06-10-2020
Reading: 
1Corinthians 6:12-20

TUESDAY 6TH OCTOBER 2020    MORNING                                          

1Corinthians 6:12-20 New International Version (NIV)

12 “I have the right to do anything,” you say—but not everything is beneficial. “I have the right to do anything”—but I will not be mastered by anything. 13 You say, “Food for the stomach and the stomach for food, and God will destroy them both.” The body, however, is not meant for sexual immorality but for the Lord, and the Lord for the body. 14 By his power God raised the Lord from the dead, and he will raise us also. 15 Do you not know that your bodies are members of Christ himself? Shall I then take the members of Christ and unite them with a prostitute? Never! 16 Do you not know that he who unites himself with a prostitute is one with her in body? For it is said, “The two will become one flesh.”[b] 17 But whoever is united with the Lord is one with him in spirit.[c]

18 Flee from sexual immorality. All other sins a person commits are outside the body, but whoever sins sexually, sins against their own body. 19 Do you not know that your bodies are temples of the Holy Spirit, who is in you, whom you have received from God? You are not your own; 20 you were bought at a price. Therefore honor God with your bodies.

Christ does not set us free so that we can do whatever we want to do; Christ sets us free so that we can do whatever God wants us to do. 


JUMANNE TAREHE 6 OKTOBA 2020     ASUBUHI                           

1WAKORINTHO 6:12-20

12 Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote vifaavyo; vitu vyote ni halali kwangu, lakini mimi sitatiwa chini ya uwezo wa kitu cho chote.
13 Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu atavitowesha vyote viwili, tumbo na vyakula. Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili.
14 Naye Mungu alimfufua Bwana, na tena atatufufua sisi kwa uweza wake.
15 Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha!
16 Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.
17 Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye.
18 Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.
19 Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;
20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.

Kristo hakutuweka huru ili tufanye lolote tunalotaka kufanya; Bali ametuweka huru ili kwamba tufanye lolote Mungu analotaka.