Date: 
07-05-2018
Reading: 
1 Thessalonians 5:16-22; (1Wathesalonike 5:16-22)

MONDAY 7TH MAY 2018 MORNING                                   

1 Thessalonians 5:16-22 New International Version (NIV)

16 Rejoice always, 17 pray continually, 18 give thanks in all circumstances; for this is God’s will for you in Christ Jesus.

19 Do not quench the Spirit. 20 Do not treat prophecies with contempt 21 but test them all; hold on to what is good, 22 reject every kind of evil.

 

At the end of his first letter to the church at Thessalonica The Apostle Paul gives some advice on how Christians should live. In a few short sentences he covers some very important issues. This week we have the theme: Pray in the name of Jesus Christ. Paul says that we should Pray continually. This means that not only should we set aside special times dedicated to prayer both on our own and with others but that our whole lives should be lived prayerfully.

Let us begin and end each day in prayer and remember to speak to God frequently throughout the day as we go about our various activities. Let us talk to Jesus about what we are doing and ask Him always to guide and help us.  

JUMATATU TAREHE 7 MEI 2018 ASUBUHI                   

1 THESALONIKE  5:16-22

16 Furahini siku zote; 
17 ombeni bila kukoma; 
18 shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu. 
19 Msimzimishe Roho; 
20 msitweze unabii; 
21 jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema; 
22 jitengeni na ubaya wa kila namna. 

Maneno haya juu ni ushauri muhimu karibu na mwisho wa Waraka wa Kwanza wa Mtume Paulo kwa Wathesalonike. Ni sentensi fupi fupi lakini ya muhimu.

Wiki hii tuna wazo kuu: Omba katika Jina la Yesu.

Mtume Paulo anaandika “ Ombeni bila kukoma”.

Maombi ni muhimu sana katika maisha ya Mkristo. Tunapaswa kuwa na wakati malumu wa kuomba peke yetu, na pamoja na  Wakristo wengine. Anza na kumaliza kila siku kwa maombi. Pia tukumbuke uwepo wa Yesu Kristo pamoja nasi wakati tupo kwenye shughuli mbalimbali za kila siku. Tumshirikishe Yesu mambo yetu na kuomba ushauri na uweza wake.