Date: 
06-04-2019
Reading: 
1 Kings 19:1-10 (1 Wafalme 19:1-10)

SATURDAY 6TH APRIL 2019 MORNING                                             

1 Kings 19:1-10 New International Version (NIV)

Elijah Flees to Horeb

1 Now Ahab told Jezebel everything Elijah had done and how he had killed all the prophets with the sword. So Jezebel sent a messenger to Elijah to say, “May the gods deal with me, be it ever so severely, if by this time tomorrow I do not make your life like that of one of them.”

Elijah was afraid[a] and ran for his life. When he came to Beersheba in Judah, he left his servant there, while he himself went a day’s journey into the wilderness. He came to a broom bush, sat down under it and prayed that he might die. “I have had enough, Lord,” he said. “Take my life; I am no better than my ancestors.” Then he lay down under the bush and fell asleep.

All at once an angel touched him and said, “Get up and eat.” He looked around, and there by his head was some bread baked over hot coals, and a jar of water. He ate and drank and then lay down again.

The angel of the Lord came back a second time and touched him and said, “Get up and eat, for the journey is too much for you.” So he got up and ate and drank. Strengthened by that food, he traveled forty days and forty nights until he reached Horeb, the mountain of God. There he went into a cave and spent the night.

The Lord Appears to Elijah

And the word of the Lord came to him: “What are you doing here, Elijah?”

10 He replied, “I have been very zealous for the Lord God Almighty. The Israelites have rejected your covenant, torn down your altars, and put your prophets to death with the sword. I am the only one left, and now they are trying to kill me too.”

Footnotes:

  1. 1 Kings 19:3 Or Elijah saw

 

The Prophet Elijah was tired and depressed because of the opposition from his enemies. But God came to encourage him and gave him food and enabled him to rest. God gave  Elijah a word to encourage him.

You might  have been going through a tough time.  Perhaps a friend or relative of yours has been experiencing various hardships. Do your best to encourage them. Let us help and support one another and let us commit our way into God’s hands so that He will lift us up in our time of need.

JUMAMOSI TAREHE 6 APRILI 2019                                        

1 WAFALME 19:1-10

 1 Basi, Ahabu akamwambia Yezebeli habari ya mambo yote aliyoyafanya Eliya, na jinsi alivyowaua manabii wote kwa upanga. 
Ndipo Yezebeli akampelekea Eliya mjumbe, kusema, Miungu wanifanyie hivyo na kuzidi, nisipokufanya roho yako kesho, panapo wakati huu, kama roho ya mmojawapo wa hao. 
Naye alipoona hayo, aliondoka, akaenda aihifadhi roho yake, akafika Beer-sheba, mji wa Yuda, akamwacha mtumishi wake huko. 
Lakini yeye mwenyewe akaendelea katika jangwa mwendo wa siku moja, akaenda akaketi chini ya mretemu. Akajiombea roho yake afe, akasema, Yatosha; sasa, Ee Bwana, uiondoe roho yangu; kwa kuwa mimi si mwema kuliko baba zangu. 
Naye akajinyosha akalala chini ya mretemu; na tazama, malaika akamgusa, akamwambia, Inuka, ule. 
Akatazama, kumbe! Pana mkate umeokwa juu ya makaa, na gudulia la maji, kichwani pake. Akala, akanywa, akajinyosha tena. 
Malaika wa Bwana akamwendea mara ya pili, akamgusa, akasema, Inuka, ule; maana safari hii ni kubwa mno kwako. 
Akainuka, akala, akanywa, akaenda katika nguvu za chakula hicho siku arobaini mchana na usiku hata akafika Horebu, mlima wa Mungu. 
Akafika kunako pango, akalala ndani yake. Na tazama, neno la Bwana likamjia, naye akamwambia, Unafanya nini hapa, Eliya? 
10 Akasema, Nimeona wivu mwingi kwa ajili ya Bwana Mungu wa majeshi; kwa kuwa wana wa Israeli wameyaacha maagano yako, na kuzivunja madhabahu zako, na kuwaua manabii wako kwa upanga; nami nimesalia, mimi peke yangu; nao wanitafuta roho yangu, waiondoe. 

Nabii Eliya alichoka sana na alitaka kukataa tama kwa sababu ya ugumu wa maisha na adui zake wengi. Mungu alisikia kilio chake. Mungu alimpa chakula na maji na alimpa usingizi. Baadaye alimtia moyo.

Inawezekana unapita mapito magumu au inawezakana rafika au ndugu yako ana msongo wa mawazo. Ni muhimu kusaidiana na kutiana moyo. Pia tulete mizigo yetu kwa Mungu ili atufariji.