Date: 
18-01-2024
Reading: 
1Nyakati 13:12-14

Alhamisi tarehe 18/01/24 asubuhi

1 Nyakati 13:12-14

12 Naye Daudi akamwogopa Mungu siku ile, akasema, Nitajileteaje sanduku la Mungu kwangu?

13 Basi Daudi hakujichukulia sanduku mjini mwa Daudi, ila akalihamisha kando na kulitia nyumbani kwa Obed-edomu Mgiti.

14 Sanduku la Mungu likakaa na jamaa ya Obed-edomu, nyumbani mwake, muda wa miezi mitatu; naye BWANA akaibariki nyumba ya Obed-edomu, na yote aliyokuwa nayo.

Mungu hubariki familia zetu

Mfalme Daudi alihifadhi Sanduku la Mungu, sanduku la Agano na Israel katika familia ya Obed-edomu. Nao wakabarikiwa wote kwani Bwana alikuwa pamoja nao. 

Nasi tukikaa pamoja na Bwana, familia zetu hubarikiwa.

Nawatakia siku njema.

C. Swai.