Date: 
04-11-2023
Reading: 
Yeremia 4:1-2

Jumamosi asubuhi tarehe 04.11.2023

Yeremia 4:1-2

1 Kama ukitaka kurudi, Ee Israeli, asema Bwana, utanirudia mimi; na kama ukitaka kuyaondoa machukizo yako, yasiwe mbele ya macho yangu, ndipo hutaondolewa;

2 nawe utaapa hivi, Kama Bwana aishivyo, katika kweli, na katika hukumu, na katika haki ndipo mataifa watajibariki katika yeye, nao watajitukuza katika yeye.

Tutengeneze mambo yaliyoharibika;

Yeremia akiwa tayari ameitika wito wa kuwa Nabii wa Mungu, anapeleka ujumbe wa Matengenezo kwa taifa la Mungu. Anapeleka ujumbe akiwataka Israeli kumrudia Bwana. Anawataka kuondoa mambo yote yaliyo machukizo mbele za Mungu. Agano la Mungu kwao ni kuwakomboa, hivyo ujumbe wa Yeremia ulilenga wakae katika Agano hilo.

Mungu aliwafikia watu wake kwa njia ya manabii wakati ule. Leo hutufikia kwa njia ya Yesu Kristo aliye Mwokozi wa ulimwengu, ambaye alikufa na kufufuka kwa ajili yetu. Huyu Kristo ndiye hutuita wakati wote kumrudia, maana ndiye Mwokozi wetu. Anakuita hata sasa. Tengeneza mambo yaliyoharibika, yaani tubu dhambi zako usamehewe, maana ufalme wa Mungu uko kwa ajili yetu. Amina.

Jumamosi njema 

Heri Buberwa