Date: 
14-09-2022
Reading: 
Mathayo 18:15-17

Jumatano asubuhi tarehe 14.09.202

Mathayo 18:15-17

[15]Na ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo.

[16]La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike.

[17]Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa; na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru.

Jirani yako ni nani?

Asubuhi ya leo tunasoma Yesu akifundisha juu ya kuonyana pale mmoja anapomkosea mwenzake. Ikilazimu kwenda mbele, Yesu anafundisha kuwaita mashahidi, na hapo ikishindikana kulihusisha Kanisa. Yesu alitaka watu wakae kwa kupatana katika hali yoyote ile, ndiyo maana akaonesha njia za kupatana.

Unapoona mtu amekukosea usiwe na hasira. Ikitokea umekasirika omba neema ya Mungu hasira iondoke. Muonye aliyekukosea, ili muendelee kupatana katika Kristo. Chuki haisaidii. 

Tunaalikwa kupendana, kusameheana na kusaidiana tunapoendelea kuishi pamoja kama Taifa la Mungu, ili ufalme wake udhihirike kwa wote.

Siku njema