Date: 
14-04-2017
Reading: 
John 11:47-53(NIV)

SATURDAY 15TH APRIL 2017 MORNING                                 

John 11:47-53  New International Version (NIV)

47 Then the chief priests and the Pharisees called a meeting of the Sanhedrin.

“What are we accomplishing?” they asked. “Here is this man performing many signs. 48 If we let him go on like this, everyone will believe in him, and then the Romans will come and take away both our temple and our nation.”

49 Then one of them, named Caiaphas, who was high priest that year,spoke up, “You know nothing at all! 50 You do not realize that it is better for you that one man die for the people than that the whole nation perish.”

51 He did not say this on his own, but as high priest that year he prophesied that Jesus would die for the Jewish nation, 52 and not only for that nation but also for the scattered children of God, to bring them together and make them one. 53 So from that day on they plotted to take his life.

The Jewish religious leaders were not happy because Jesus was very popular. Many people were following Jesus and listening to His teachings. The Jewish religious leaders were used to having prestige and authority over the people. They didn’t want to lose their position. So they plotted to kill Jesus.

Are you concerned with what is true or just what is convenient and comfortable?  The message of the Gospel is very demanding. Will you follow Christ even when it is hard to do so? 

JUMAMOSI TAREHE 15 APRILI  2017 ASUBUHI               YOHANA 11:47-53

Yohana 11:47-53

47 Basi wakuu wa makuhani na Mafarisayo wakakusanya baraza, wakasema, Tunafanya nini? Maana mtu huyu afanya ishara nyingi. 
48 Tukimwacha hivi, watu wote watamwamini; na Warumi watakuja, watatuondolea mahali petu na taifa letu. 
49 Mtu mmoja miongoni mwao, Kayafa, aliyekuwa Kuhani Mkuu mwaka ule, akawaambia, Ninyi hamjui neno lo lote; 
50 wala hamfikiri ya kwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, wala lisiangamie taifa zima. 
51 Na neno hilo yeye hakulisema kwa nafsi yake; bali kwa kuwa alikuwa Kuhani Mkuu mwaka ule, alitabiri ya kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa hilo. 
52 Wala si kwa ajili ya taifa hilo tu; lakini pamoja na hayo awakusanye watoto wa Mungu waliotawanyika, ili wawe wamoja. 
53 Basi tangu siku ile walifanya shauri la kumwua. 
 

Viongozi wa dini ya Kiyahudi walikuwa na wivu dhidi ya Yesu. Mafundisho na miujiza ya Yesu Kristo yaliwavuta wengi. Hawa viongozi waliona kama heshima yao imepungua. Walitaka kumua Yesu.  Hawajajali kujua kama ujumbe wake ni kweli au siyo. Walijali tu nafasi zao na heshima yao.

Sisi je! Tunatafuta ukweli au tunahitaji unafuu wa maisha ?

Utamfuata Yesu hata kama ni ngumu?