Sikukuu ya Mikaeli na Watoto 2024 | Azania Front Cathedral
Siku ya Jumapili tarehe 29 Septemba 2024 katika Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front ilifanyika Sikukuu ya Mikaeli na Watoto; Sikukuu ambayo hufanyika kila mwaka kwa ajili ya kumkumbuka malaika Mikeli na watakatifu wote pamoja na watoto. Ibada hii hufanyika kwa kuongozwa na watoto wakisaidiana na walimu wao pamoja na watumishi wengine wa usharika (parish workers).