Date: 
24-02-2022
Reading: 
1 Samweli 17:46-50

Ailhamisi asubuhi tarehe 24.02.2022

1 Samweli 17:46-50

46 Siku hii ya leo Bwana atakuua mkononi mwangu, nami nitakupiga, na kukuondolea kichwa chako, nami leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya majeshi ya Wafilisti, ili kwamba dunia nzima wajue ya kuwa yuko Mungu katika Israeli.

47 Nao jamii ya watu wote pia wajue ya kwamba Bwana haokoi kwa upanga wala kwa mkuki; maana vita ni vya Bwana, naye atawatia ninyi mikononi mwetu.

48 Ikawa, hapo Mfilisti alipojiinua, akaenda akamkaribia Daudi, ndipo Daudi naye akapiga mbio, akalikimbilia jeshi ili akutane na yule Mfilisti.

49 Daudi akatia mkono wake mfukoni, akatwaa humo jiwe moja, akalitupa kwa kombeo lake, akampiga Mfilisti katika kipaji cha uso; jiwe hilo likamwingilia kipajini, akaanguka chini kifudifudi.

50 Hivyo Daudi akamshinda yule Mfilisti kwa kombeo na jiwe, akampiga Mfilisti, akamwua; walakini Daudi hakuwa na upanga mkononi mwake.

Neno la Mungu lina nguvu;

Leo asubuhi tunamuona Goliath akiuawa na Daudi, tena kwa jiwe kwenye kombeo! Goliati alikuwa tishio, jitu kubwa linalotisha! Alisema atawapiga Israeli na watakuwa watumishi wa wafilisti. Akasema kinyume chake ikitokea, basi wafilisti wawe watumishi wa Israeli. Kumbe Mungu alikuwa upande wa Israeli, Goliati akafa yeye. 

Daudi alimshinda Goliati kwa msaada wa Bwana. Mstari wa 46 unaonesha jambo hili, kuwa Daudi alimtegemea Bwana. Kumbe nasi tukimtegemea Bwana, kwa nguvu ya neno lake tunaweza kuyakabili yote yanaoonekana hayawezekani. 

Siku njema.