Date: 
11-03-2019
Reading: 
1 Peter 3:13-17

MONDAY 11TH MARCH 2019

1 Peter 3:13-17 New International Version (NIV)

13 Who is going to harm you if you are eager to do good? 14 But even if you should suffer for what is right, you are blessed. “Do not fear their threats[a]; do not be frightened.”[b] 15 But in your hearts revere Christ as Lord. Always be prepared to give an answer to everyone who asks you to give the reason for the hope that you have. But do this with gentleness and respect, 16 keeping a clear conscience, so that those who speak maliciously against your good behavior in Christ may be ashamed of their slander. 17 For it is better, if it is God’s will, to suffer for doing good than for doing evil.

Footnotes:

  1. 1 Peter 3:14 Or fear what they fear
  2. 1 Peter 3:14 Isaiah 8:12

To better understand today's passage, read from verse 8. The general message is 'to be ready to suffer for doing good' for there will be those who persecute you for doing right. We are not to fear threats or be frightened in the quest for doing right but revere Christ as Lord. May God help us to stay in the right course even when we are persecuted?

JUMATATU TAREHE 11 MACHI 2019

1PETRO 3:13-17

13 Naye ni nani atakayewadhuru, mkiwa wenye juhudi katika mema?
14 Lakini mjapoteswa kwa sababu ya haki mna heri. Msiogope kutisha kwao, wala msifadhaike; bali mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu.
15 Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu.
16 Nanyi mwe na dhamiri njema, ili katika neno lile mnalosingiziwa, watahayarishwe wale wautukanao mwenendo wenu mwema katika Kristo.
17 Maana ni afadhali kuteswa kwa kutenda mema, ikiwa ndiyo mapenzi ya Mungu, kuliko kwa kutenda mabaya.

Ujumbe wa mistrari ya hapo juu kwa jumla ni 'Kuwa tayari kuteseka kwa kutenda mema' Ili kuelewa vizuri kifungu cha leo, soma kutoka mstari wa 8. Katika maisha yetu kutakuwa na wale wanaokutesa kwa kutenda haki. Hatupasi kuogopa vitisho au kuwa na hofu katika jitihada za kutenda haki, bali ni kumheshimu Kristo kama Bwana. Mungu atusaidie tuendelee katika njia sahihi hata tunapokutana na mateso.