Date: 
13-05-2023
Reading: 
Zaburi 138:1-8

Hii ni Pasaka 

Jumamosi asubuhi tarehe 13.05.2023

Zaburi 138:1-4

1 Nitakushukuru kwa moyo wangu wote, Mbele ya miungu nitakuimbia zaburi.

2 Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu, Nitalishukuru jina lako, Kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako, Kwa maana umeikuza ahadi yako, Kuliko jina lako lote.

3 Siku ile niliyokuita uliniitikia, Ukanifariji nafsi kwa kunitia nguvu.

4 Ee Bwana, wafalme wote wa dunia watakushukuru, Watakapoyasikia maneno ya kinywa chako.

Kila aliye hai amsifu Bwana;

Katika Zaburi tunayoisoma leo asubuhi, mwimbaji anamshukuru Mungu kwa moyo wote. Anatambua fadhili na uaminifu wa Mungu, hivyo kumshukuru wakati wote. Mwimbaji anaendelea kumtegemea Bwana akimuomba asimuache daima kama anavyomalizia Zaburi;

Zaburi 138:8

Bwana atanitimilizia mambo yangu; Ee Bwana, fadhili zako ni za milele; Usiziache kazi za mikono yako.

Zaburi ya asubuhi ya leo inatukumbusha kuishi maisha ya shukrani kwa Mungu. Tunawajibika kumshukuru Mungu kila wakati na kumuomba atubariki siku zote za maisha yetu.

Tumshukuru Mungu, tuombe asituache, na azibariki kazi za mikono yetu.

Jumamosi njema 

Heri Buberwa