Date: 
11-05-2023
Reading: 
Zaburi 59:16-17

Hii ni Pasaka 

Alhamisi asubuhi tarehe 11.05.2023

Zaburi 59:16-17

16 Nami nitaziimba nguvu zako asubuhi, Nitaziimba fadhili zako kwa furaha. Kwa kuwa ndiwe uliyekuwa ngome yangu, Na makimbilio siku ya shida yangu.

17 Ee nguvu zangu, nitakuimbia kwa furaha, Maana Mungu ndiye aliye ngome yangu, Mungu wa fadhili zangu.

Kila aliye hai amsifu Bwana;

Mwimbaji wa Zaburi tunayoisoma asubuhi hii anamkiri Bwana kuwa ngome yake na kimbilio wakati wa shida, hivyo analiona hitaji la kuimba sifa za Bwana. Zaburi nzima inaonesha mwimbaji akiomba neema ya Mungu, na mwisho anahitimisha kwa kuuona utukufu wake na kumsifu daima.

Mungu ndiye kimbilio letu katika kazi zetu za kila siku. Ni muhimu kukimbilia ulinzi wake. Tunapomtegemea katika maisha yetu tunatenda atakayo. Na hapo ndipo anakuwa ngome yetu. Tuishi kwa kutenda yaliyo mapenzi yake, huo ndiyo utume mwema.

Siku njema.

 

Heri Buberwa