Date: 
09-05-2023
Reading: 
Matendo 16:25-30

Hii ni Pasaka 

Jumanne asubuhi tarehe 09.05.2023

Matendo ya Mitume 16:25-30

25 Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza.

26 Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa.

27 Yule mlinzi wa gereza akaamka, naye alipoona ya kuwa milango ya gereza imefunguka, alifuta upanga, akataka kujiua, akidhani ya kuwa wafungwa wamekimbia.

28 Ila Paulo akapaza sauti yake kwa nguvu, akisema, Usijidhuru, kwa maana sisi sote tupo hapa.

29 Akataka taa ziletwe, akarukia ndani, akitetemeka kwa hofu, akawaangukia Paulo na Sila;

30 kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka?

Kila aliye hai amsifu Bwana;

Paulo na Sila waliwekwa gerezani kwa sababu ya kuhubiri habari za Yesu Kristo. Wakiwa gerezani usiku waliimba nyimbo za kumsifu Mungu, likatokea tetemeko la nchi hadi msingi wa gereza kutikisika. Gereza lilifunguka wakatoka. Askari aliogopa akataka kujiua, lakini Paulo akamzuia.

Tunachokiona ni kuwa sifa za akina Paulo zilisababisha gereza likafunguka. Yaani walitoka gerezani kwa njia ya sifa kwa Bwana. Nasi tunaalikwa kumsifu Bwana wakati wote. Tunamsifu Bwana kwa kuishi tukitenda yaliyo mapenzi yake, na hapo ndipo hutuokoa na kutusaidia katika njia zetu.

Siku njema.

Heri Buberwa