Date: 
06-05-2023
Reading: 
Yohana 17:13-14

Hii ni Pasaka 

Jumamosi asubuhi tarehe 06.05.2023

Yohana 17:13-14

13 Na sasa naja kwako; na maneno haya nayasema ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao.

14 Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.

Maisha mapya ndani ya Yesu.

Sura ya 17 ni sala ndefu aliyosali Yesu, iliyoandikwa. Katika sala hii aliwaombea umoja watu wake. Aliwaombea wamjue yeye aliye kweli, na hiyo kweli iwaokoe. Sehemu tuliyosoma, Yesu anawaombea watu wake furaha katika yeye. Yesu anasema amewapa watu wake neno lake, nao hao watu siyo wa ulimwengu, bali ni wa kwake.

Sehemu ya sala ya Yesu asubuhi hii inasema ametupa neno lake, sisi ni wa kwake. Tutafakari kama hilo neno tunalisoma na kulishika. Tukilishika neno lake tunakuwa wake, na maisha yetu yanakuwa mapya wakati wote. Jumamosi njema.

 

Heri Buberwa