Date: 
03-05-2023
Reading: 
Warumi 15:3-8

Hii ni Pasaka 

Jumatano asubuhi 03.05.2023

Warumi 15:8-13

8 Kwa maana nasema, ya kwamba Kristo amefanyika mhudumu wa agano la kutahiriwa kwa ajili ya kweli ya Mungu, kusudi azithibitishe ahadi walizopewa baba zetu;

9 tena ili Mataifa wamtukuze Mungu kwa ajili ya rehema zake; kama ilivyoandikwa, Kwa hiyo nitakushukuru kati ya Mataifa, Nami nitaliimbia jina lako.

10 Na tena anena, Furahini,Mataifa,pamoja na watu wake.

11 Na tena, Enyi Mataifa yote,msifuni Bwana; Enyi watu wote,mhimidini.

12 Na tena Isaya anena, Litakuwako shina la Yese, Naye aondokeaye kuwatawala Mataifa; Ndiye Mataifa watakayemtumaini.

13 Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu.

Maisha mapya ndani ya Yesu;

Mtume Paulo anawaandikia Warumi kwamba Kristo ndiye Agano la kweli katika kutimiza ahadi za Mungu. Aliwataka wajue kuwa Yesu ndiye ukamilifu wa torati. Kristo anadhihirika kama Mwokozi wa ulimwengu astahiliye sifa. Paulo anawaita watu wamsifu Bwana, lakini wadumu katika yeye aliye ukamilifu wa Agano la Mungu katika kuuomboa Ulimwengu 

Tunachokiona asubuhi hii ni kuwa Yesu Kristo ndiye mwenye ukamilifu wote katika kuukomboa ulimwengu. Tuwe wahudumu wa Kristo kama Paulo anavyosema, ili maisha yetu yawe mapya katika yeye siku zote. Amina.

Siku njema.

 

Heri Buberwa 

Mlutheri