Date: 
14-12-2022
Reading: 
Luka7:27

Hii ni Advent 

Jumatano asubuhi tarehe 14.12.2022

Luka 7:27

[27]Huyo ndiye aliyeandikiwa haya, 

Tazama, namtuma mjumbe wangu 

Mbele ya uso wako, 

Atakayeitengeneza njia yako mbele yako.

Bwana anawafariji watu wake;

Yohana alikuwa amefungwa gerezani akasikia habari za Yesu. Ndipo akawatuma wanafunzi wake (Yohana) kumuuliza Yesu kwamba yeye ndiye Masihi au atazamiwe mwingine? Yesu akawajibu wanafunzi wa Yohana kwamba wakamwambie mambo yanayotendeka, wagonjwa wanapona, neno linahubiriwa, vipofu wanaona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa.

Wanafunzi wa Yohana walipoondoka, Yesu akaanza kuwaeleza makutano habari za Yohana. Kwamba huyu ndiye aliyenenwa na manabii, akimnukuu Nabii Malaki;

Malaki 3:1

[1]Angalieni, namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu; naye Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu lake ghafula; naam, yule mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, anakuja, asema BWANA wa majeshi.

Alikuwa anaeleza habari za Yohana ambaye wapo ambao hawakumwamini. 

Lakini Yohana alileta ujumbe wa watu kujiandaa kumpokea Yesu. Aliwaita watu kutubu na kubatizwa, akisema ufalme wa Mungu umekaribia. Tunakumbushwa ujumbe wa Yohana Mbatizaji, kwamba tuandae mioyo yetu kumpokea Yesu ambaye anakuja kulichukua Kanisa lake. Amina.

Jumatano njema