Azaniafront Cathedral yaadhimisha Sikukuu ya Mavuno 2021

Siku ya Jumapili, tarehe 24/10/2021, Usharika wa KKKT Kanisa Kuu Azaniafront Cathedral umefanya maadhimisho ya sikukuu ya mavuno, sikukuu ambayo hufanyika kila mwaka ili kutoa fursa kwa washarika kumtolea Mungu sehemu ya matunda au mavuno ya kazi wanazozifanya.

Ibada ya kusherehekea sikukuu hii ya mavuno kwa mwaka 2021 imefanyika katika viwanja vya usharika wa Kanisa Kuu Azaniafront huku ikihudhuiriwa na washarika waliojitokeza kwa wingi wakiwa na mavuno yao tayari kwa kumtolea Mungu.