JUMATATU TAREHE 25 OKTOBA 2021, ASUBUHI
Wagalatia 6:8-10
8 Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele.
9 Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho.
10 Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.
Tukaze mwendo katika Yesu Kristo;
Mtume Paulo anawaandikia Wagalatia akiwausia kutenda mema bila kuchoka. Anawaambia wasipande katika mwili, bali katika Roho ambapo mavuno yake ni uzima wa milele.
Tuepuke kupanda katika mwili, yaani tuwe na imani ya kweli pasipo kuyumbishwa na dhambi. Tukipanda kwa Roho Mtakatifu, hutuwezesha kutenda mema, hivyo kuurithi uzima wa milele.
Nakutakia wiki njema, yenye ushuhuda na mafanikio.
MONDAY 25TH OCTOBER 2021, MORNING
Galatians 6:8-10 (NIV)
8 Those who live only to satisfy their own sinful nature will harvest decay and death from that sinful nature. But those who live to please the Spirit will harvest everlasting life from the Spirit. 9 So let’s not get tired of doing what is good. At just the right time we will reap a harvest of blessing if we don’t give up. 10 Therefore, whenever we have the opportunity, we should do good to everyone—especially to those in the family of faith.
Let us press on in Jesus Christ;
The apostle Paul writes to the Galatians advising them to do good without tiring out. He tells them not to sow in the flesh, but in the Spirit, whose harvest is eternal life.
Let us avoid sowing in the flesh, that is, having true faith without being swayed by sin. If we sow by the Holy Spirit, it enables us to do good, thus inheriting eternal life.
I wish you a good week, with testimonials and success.