Kwaya ya Agape, ni kwaya ya uinjilisti inayomhubiri kristo kwa njia ya uimbaji.
Kwaya hii ilianzishwa katika kanisa kuu Azania Front Cathedral mnamo mwaka 2002 ikiwa na wanakwaya 12, mwenyekiti akiwa Allen David, Katibu Fritz Msanjo,
Mwalimu Kiongozi Amri Hingi, Mweka hazina Cesilia K. Hingi, mwenyekiti wa Uinjilisti dada Gladness Maleko.

Kwaya hii inaongozwa kwa kufuata mwongozo uliotungwa na wanakwaya wenyewe katika misingi ya kuanzisha kwaya hii. Kwa mujibu wa mwongozo wa agape kuna ngazi sita za uongozi unaochaguliwa na mkutano mkuu, ambazo ni Mwenyekiti wa
kwaya, Katibu wa kwaya, Mweka hazina, Bibi/bwana nidhamu, mwenyekiti idara ya mipango na mwenyekiti idara ya uinjilisti

Kwa muda wa miaka 11 sasa kwaya imekuwa na awamu tatu za uongozi na hivi sasa kwaya inaongozwa na:

  1. Allen David Mwenyekiti (aliyechaguliwa kwa mara nyingine kushika wadhifa huu kwa kipindi cha miaka minne kuanzia 2011).
  2. Mosses Kombe - Katibu
  3. Adella Kaale -Mweka hazina
  4. Godfrey Moshi - Mwalimu kiongozi, (ambaye pia ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa awamu ya Pili.)
  5. Michael Nkya - Mwenyekiti wa mipango
  6. Irene M. Moshi - Bibi nidhamu.
  7. Peter Mlagha – Kaimu mwenyekiti idara ya Uinjilisti.

Huduma za kwaya.
Kwaya imeendelea kukuwa na kupokea waimbaji wa rika mbali mbali kuanzia wanafunzi wa sekondari, wa vyuo, wafanyakazi, wafanya biashara na watu wa kada zote.
Kwaya imehudumu kwa njia ya uimbaji na maigizo katika maeneo mbali mbali ndani nan je ya nchi. 
 

Group Articles

Agape wakiimba katika ibada nyimbo zilizo kwenye CD
Wanakwaya wa Agape Evangelical Singers wakiwa wanaondoka Kanisa kuu Azania front kuelekea Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere tayari kwa safari ya uinjilisti mkoani Arusha.