Date: 
23-10-2021
Reading: 
Marko 10:35-44

Jumamosi asubuhi 23.10.2021 

Marko 10:35-44

[35]Na Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, wakamwendea, wakamwambia, Mwalimu, twataka utufanyie lo lote tutakalokuomba.

[36]Akawaambia, Mwataka niwafanyie nini?

[37]Wakamwambia, Utujalie sisi tuketi, mmoja mkono wako wa kuume, na mmoja mkono wako wa kushoto, katika utukufu wako.

[38]Yesu akawaambia, Hamjui mnaloliomba. Mwaweza kunywea kikombe ninyweacho mimi, au kubatizwa ubatizo nibatizwao mimi?

[39]Wakamwambia, Twaweza. Yesu akawaambia, Kikombe ninyweacho mimi mtakinywea, na ubatizo nibatizwao mimi mtabatizwa;

[40]lakini habari ya kuketi mkono wangu wa kuume au mkono wangu wa kushoto si langu kuwapa, ila wao watapewa waliowekewa tayari.

[41]Hata wale kumi waliposikia wakaanza kuwakasirikia Yakobo na Yohana.

[42]Yesu akawaita, akawaambia, Mwajua ya kuwa wale wanaohesabiwa kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha.

[43]Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu anayetaka kuwa mkubwa kwenu, atakuwa mtumishi wenu,

[44]na mtu anayetaka kuwa wa kwanza wenu, atakuwa mtumwa wa wote.

Njia ya ufalme wa Mungu;

Yakobo na Yohana (wana wa Zebedayo) waliomba kukaa na Yesu, mmoja kulia, mwingine kushoto katika ufalme wake. Yesu aliwaambia kuwa ufalme wake ni kwao waliowekewa tayari.

Tunaishi maisha ya Kikristo tukienda ibadani na kushiriki kazi za kijamii na Kanisa kwa ujumla, lakini je, ufalme wa Mungu upo kwa ajili yetu? Maisha yetu yaakisi ukristo wa kweli, ambao katika imani hiyo tutaingia katika ufalme wa Mungu.

Jumamosi njema.