Date: 
21-10-2021
Reading: 
1 Wathesalonike 2:9-12

Alhamisi asubuhi 21.10.2021

1 Wathesalonike 2:9-12

[9]Maana, ndugu, mnakumbuka taabu yetu na masumbufu yetu; kwa kuwa mchana na usiku tulifanya kazi tusije tukamlemea mtu wa kwenu awaye yote, tukawahubiri hivi Injili ya Mungu.

[10]Ninyi ni mashahidi, na Mungu pia, jinsi tulivyokaa kwenu ninyi mnaoamini, kwa utakatifu, na kwa haki, bila kulaumiwa;

[11]vile vile, kama mjuavyo, jinsi tulivyomwonya kila mmoja wenu kama baba awaonyavyo watoto wake mwenyewe, tukiwatia moyo na kushuhudia;

[12]ili mwenende kama ilivyo wajibu wenu kwa Mungu, mwenye kuwaita ninyi ili mwingie katika ufalme wake na utukufu wake.

Njia ya ufalme wa Mungu;

Mtume Paulo anaelezea huduma yake katika Thesalonike jinsi alivyofanya kazi bila kuchoka, kwa bidii ili kuwaleta watu kwa Yesu. Paulo aliwaonya watu wa Thesalonike na kuwashuhudia habari za Kristo, ili wawe watoto wa Mungu, katika ufalme wake.

Tuyaige maisha ya Paulo, ya uaminifu katika kazi ya Mungu. Yeye aliifanya kazi ya Mungu kwa uaminifu. Nasi tukifanya hivyo, wengi watakuja kwa Yesu, hivyo tutakuwa tumeshiriki kuujenga ufalme wake, kwa ajili ya wote.  

Siku njema.